FBME Yasema Asante kwa ‘Wadau’

Septemba 3, 2014

FBME Limited ilituma ujumbe wa shukrani kwa wale watu mbalimbali na mashirika ambayo wamejitokeza kutoa msaada kwa Benki katika mapambano yake dhidi ya Azimio na hatua zilizowekwa dhidi ya tawi la Cyprus. Kuna uvumi wa wazi ulioenea kwa umma kwamba hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus zimekuwa za haraka sana, si za haki na zenye madhara makubwa. Kuna ukimya wa kimataifa kuhusu matendo ya mamlaka ya benki ya Cyprus dhidi ya tawi la benki ya kigeni, wakati hatua hizo zimechukuliwa bila kushauriana na Mwangalizi Mkuu aliyepo Makao makuu nchini Tanzania.