Monthly Archives: Januari 2015

Mafunzo ya Kuzuia Utakatisishaji wa Fedha haramu na Kufadhili Ugaidi (AML na CTF)

Januari 23, 2015

Kama sehemu ya ahadi yake kwa FinCEN, Benki ya FBME itafanya upya mafunzo kwa wafanyakazi ili kuonyesha ahadi yake ya utekelezaji wa udhibiti wa mifumo ya benki wakati wote. Mafunzo haya mapya yataongeza elimu ambayo tayari wafanyakazi wanayo na itazidisha mifumo ya udhibiti wa Benki. Lengo hasa ni sera ya kukabiliana na kupambana na fedha haramu, jua-mteja-wako, kukabiliana na kufadhili ugaidi na vikwazo vya kiuchumi.

Continue reading

Jopo la Usuluhishi ICC Laundwa

Januari 26, 2015

 Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara  mjini Paris imekubaliana juu ya uteuzi wa jopo la wasuluhishi walioteuliwa na wamiliki wa Benki ya FBME, Jamhuri ya Cyprus na mwenyekiti wa mahakama. Moja ya kazi ya kwanza kwa wasuluhishi hao ni kuangalia kwa haraka suala la madhara yaliyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus kufuatia kukubaliwa kwa shauri la usuluhishi na ICC tarehe 28 Oktoba 2014.

Continue reading

Benki ya FBME na FinCEN Wajadiliana

Januari 23, 2015

Tarehe 21 Januari, mkutano ulifanyika jijini Washington DC kati ya wawakilishi wa Benki ya FBME na Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN. Lengo lilikuwa kujadili zaidi Notisi ya Matokeo ya FinCEN (NOF) na Ilani ya Mapendekezo (NPRM), iliyochapishwa kwenye Daftari la Shirikisho tarehe 22 Julai 2014, na majibu ya Benki ya FBME ya masuala yaliyoorodheshwa kwenye Notisi hizo.

Continue reading

Msimamizi Afikia Kiwango Kipya

Desemba 31, 2014

Kiwango cha malipo ya kila siku kimepunguzwa hadi EUR 1,000 kwa siku, kulingana na amri iliyotolewa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus, Dinos Christofides. Kwa nini amepunguza kiwango – kilichowekwa mwanzoni EUR10,000, kisha kikawa EUR 5,000 hivi karibuni kufikia EUR 2,000 – hajaamua kushirikiana nasi. Kuna mamilioni ya Euro yaliyopo katika Benki Kuu ya Cyprus (ambayo FBME inaendelea kulipa adhabu) na hakuna hatari ya benki kuwa mufilisi. Ni nini haswa malengo yake?

Continue reading

Wafanyakazi wa FBME Wachangia Familia

8 Januari, 2015

Wafanyakazi wa Benki ya FBME na Kitengo cha Kadi cha FBME kwa mwezi Disemba wamejitolea michango ya chakula na vitu vingine kwa familia zenye uhitaji kwenye mpango wa kila mwaka wa kusaidia familia. Mbali na chakula, wafanyakazi hao wamekusanya nguo, mashuka na vitu vingine vya majumbani, wakati wengine wametoa fedha taslimu zilizotumika kununulia vitu mbalimbali. Familia zenye uhitaji zinatambuliwa na mpango huu maalum. Wafanyakazi wa Benki ya FBME na wa Kitengo cha Kadi wamekuwa wakijitolea kwenye mpango huu wa kusaidia familia zenye uhitaji kwa miaka mitatu mfululizo kama sehemu ya mpango mkubwa wa Ujirani Mwema unaofanywa kwa niaba ya Benki.

Heri ya mwaka mpya 2015

Desemba 31, 2014

Wamiliki wa FBME Limited wanatuma salaam za heri za mwaka 2015 kwa wafanyakazi, wateja, wafuasi, marafiki,  wachambuzi na wale wote ambao wameisaidia FBME katika mapambano yake dhidi ya udhalimu, uzembe, udanganyifu na vitendo vingi vya mashaka.

Ni matumaini yetu kuwa Mwaka Mpya utaleta habari njema zaid!