JUMUIYA

JUMUIYA – wajibu wetu wa kijamii

Sisi, watu wa FBME Limited, tunaamini kuwa shirika lolote lazima litoe ama lisaidie jamii ambayo iliopo na inapofanyia shughuli zake. Lengo la biashara ni kuhudumia jamii, kuwaajiri na kutumia werevu ili kuweza kuboresha maisha ya watu wanaotuzunguka. Vilevile tunaamini kuwa ni muda sahihi kuweka mambo sahihi na tofauti ya kubaki ulivyo na kuwa kuwa unaetaka kuwa ni kufanya kazi kwa bidii zaidi!

Tukiangalia rekodi zetu za mwaka 1998, kampuni yetu FBME Ltd imeshatoa jumla ya €756,463.12 katika misaada kwa wanaostahili mjini Cyprus.

Hapa chini tunaelezea baadhi ya michango ya udhamini kutoka FBME

 “Maonyesho ya mashine Leonardo Da Vinci” 2013

Kufadhaliwa kwa maonyesho hayo ilikuwa pamoja na kusherehekea maadhimisho ya miaka 30 ya uwepo wa FBME katika kisiwa hicho.
Maonyesho hayo yanachukuliwa kuwa moja ya maonyesho ya mafanikio zaidi yanayofanyika katika mji wa Cyprus, yalibahatika kuwemo ndani ya kipindi cha maadhimisho ya miaka 30 ya uwepo FBME Ltd kisiwani hapo, yalifungwa milango yake tarehe 28 Februari. Zaidi ya watu kumi na nane elfu walihudhuria, elfu saba kati yao walitokana na makundi ya wanafunzi , ambao walipata nafasi ya kutembelea maonyesho ya kipekee.
Maonyesho yalifunguliwa kuanzia tarehe 3 Januari hadi 28 Februari 28 kwenye ukumbi wa Evagoras Lanitis, katika mji wa Limassol madhumuni yakiwa kuwafahamisha wageni sehemu iliokuwa haijulikani ya Da Vinci, umahirii wa akili zake katika sekta ya mashine.

Mashine hizo zilionyeshwakatikasehemu nne; kijeshi, haidroliki na bahari,mitambo ya kuruka na mashine za kanunirahisi za umakanika.Wageni waliweza kugundua upande wa uhandisi na uvumbuzi wa Da Vincikwani mifano zaidi ilionyeshwa yenyemuingiliano.

Zaidi ya wageni 18,000 walipata mwanga juu ya vilivyoundwa, ambavyo vinajumuisha pamoja na mambo mengine, aligundua gearbox, mashine ya meli iitwayo Hull, jeki ya kisasa ya gari, glider na parashuti, na kuweka mazingira kwa ajili ya uvumbuzi wa helikopta na gari za kijeshi ya kivita.

Katika uzinduzi rasmi wa maonyesho hayo Mwenyekiti wa FBME Ltd alisema “Tunapaswa kutoa kwa jamii ambayo sisi tunapofanyia kazi”, na hivi leo, Benki inaweza kujigamba na kutangaza kwamba wameweza kukusanya michango ambayo itazidi Eur 100,000 kwa ajili ya Hospitali ya watoto ya Askofu Mkuu III Makarios.

JIPYA: Kiasi ambacho kilichokusanywa kwenye maonyesho ya Da Vinci hadi mwisho, kutokana na mipango ya Benki ni takriban € 130,000. Tarehe 9 Julai 2014, uongozi wa Benki ulikutana na Dk Petros Matsas, Daktari na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Askofu Mkuu Makarios III, mkutano ambao makandarasi na washirika wa mradi walipewa maelekezo ya kuanza kazi, uamuzi ambao hii leo umebatilishwa kwa sababu ya maendeleo yalioikumba benki.

Mbio za Kimataifa za Limassol

Ni jambo linalofahamika kuwa miradi ya Corporate hutumika katika majukumu ya kijamii na hasa hutumika katika udhamini wa michezo kama chombo ili kufikia malengo ya shirika, kwa sababu kuu mbili. Kwanza, michezo huweza kuleta mabadiliko ya kweli ya maisha yetu, kwa mtu kushiriki ama kuwa muangaliaji na mshangiliaji, na pili, mazoezi ya viungo katika kila ngazi ya binadamu; kutoka kwa watoto kucheza mpira wa miguu mitaani, matukio makubwa duniani kama vile Kombe la Dunia la FIFA, michezo ya Olimpiki, hata pia Marathon Limassol.

“Afya katika akili ni afya katika mwili”! Usemi huu wa Kigiriki uliogunduliwa miaka 1000 iliopita, usemi huu umehibitishwa sasa baada ya utafiti wa kisayansi na umeonyesha uwiano wa juu kabisa. Katika usimamizi wa huduma kwa jamii, michezo ni moja ya nguzo za FBME Benk katika programu zake. FBME Ltd ni mdhamini na inajifaharisha kuwa mdhamini wa mbio hizo yanayo julikana kama “Mbio za km 5 za FBME Bank”. Lengo la Benki ni kuhamasisha ushiriki katika matukio ya michezoili kuboresha afya zetu, na hatimae ubora wa maisha yetu.

Mbio za kimataifa za 8, ni moja ya matukio muhimu na makubwa mjini Cyprus, yalifanyika Machi 16 mwaka huu. Ushiriki wa mwaka huu ulikuwa wa aina yake kwani zaidi ya wakimbiaji 70 kutoka mjini Cyprus na nje ya nchi walishiriki katika “maadhimisho ya mchezo na yenye motisha “. Mbio zilizokuwa maarufu katika jamii zote mbio za “Km 5 za mbio za jamii ya FBME Benk” Makampuni 120 mengine yalishiriki na wakimbiajiwalikuwa 5000. Kwa muda wa miaka miwili mfululizo, FBME Ltd imefadhili mbio hizo.

Kwa mara nyingine tena, tukio la mwaka huu, limeleta hisia za uamuzi, shauku na ushirikiano wa timu; tamasha la michezo hii ilikuwa mizuri sana, FBME limited kwa hakika ilifurahi kwa kushiriki kama mdhamini wa tamasha kubwa kama hili.

Mbio za 6 za km 10 za FBME Benki

Mbio za 6 FBME Benki za urefu wa km 10 za mwaka 2013 zilikuwa na usemi ”Kiembeni nasi kwa ajili ya watoto wetu “, FBME inajigamba kufadhali mbio hizo ambazo zilifanyika tarehe 16 Novemba katika uwanja wa taifa Athalassa mjini Nicosia. Mazingira mazuri na hifadhi ya asili katika ya eneo hilo yalizidisha ubora wa burudani na tukio hilo.

Mbali na hilo la kuhamasisha ushiriki wa matukio ya michezo ambayo huboresha afya zetu na hivyo ubora wa maisha yetu, tukio hili pia lilikuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya FBME Ltd ili kuongeza juhudi kwa ajili ya ujenzi wa wadi ya watoto katika Hospitali ya Arch. Makarios III mjini Nicosia.

Mbali na matukio ya mbio, washiriki walipata fursa ya kushiriki katika shughuli nyingine ambazo ni pamoja na kuchukua picha na pikipiki ya awali ya Harley Davidson, uchoraji wa uso na kushiriki katika vikao vya yoga.

Meli ya Kyrenia-Liberty

Mnamo mwaka 2001, ujenzi wa majaribio wa pili wa meli ifananayo na meli ya kale ya Kyrenia, “Kyrenia-Liberty” ilizuiwa wakati mmiliki wa meli Kerynia-Chrysocava”, alipopata matatizo ya kifedha. Paundi 20,000 za Cyprus zilihitajika kwa haraka kumalizia mradi ili kuwezesha meli –ipate fursa ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki mwaka 2004 mjini Athens.

Taasisi ilifanya juhudi mbalimbali ili kupata fedha kutoka Serikali, taasisi nyingine pamoja na Usharika wa mabenki ya Cyprus , lakini hakuna kilichofanikiwa.

FBME Ltd, bila kusita, iliamua kufadhili mradi huu; waliomba kibali kutoka Benki Kuu ya Cyprus, na kuhakikisha kuwa wamefuata taratibu za kisheria. Ombi lao lilipokataliwa, mmoja wa wanahisa wa FBME Ltd, alitoa kiasi chote kilichohitajika yaani jumla ya paundi 20,000 za Cyprus kutoka kwenye akaunti yake binafsi, ili kuwezesha kukamilisha meli “Kyrenia-Liberty”. Tunaamini kwa kuwepo kwa tukio hili la michezo hayo hapa nyumbani na kutokana na ufadhili, ukarimu na mchango huu, meli iliweza kusafiri kwenda Athens ikiwa imepakia shehena ya shaba kwa ajili ya medali ya shaba.

Msaada waenda “Kituo cha Counseling cha wanajamii wanao fuata Monastery ya Mtakatifu wa Kykkos

Jumla ya Euro 30,000 zilitolewa kwa kituo cha Monastery ya Mtakatifu Kykkosili kusaidia familia zenye haja na shida. Walipewa vocha za € 50 za chakula zenye thamani ya Euro 25,000 (hizi hazikuwa na alama wala nembo ya Benki) na iliyobaki € 5,000 waliwekewa kwenye akaunti yao ya benki ili waweze kuwalipia bili za maji, simu na umeme hizo familia zilizokuwa wahitaji.

Masomo ya Yoga yatolewa bure

Kama sehemu ya mchango wa FBME kwa jamii, kwa miaka mitatu iliyopita, Benki ya imetoa masomo ya yoga si tu kwa wafanyakazi wake bali pia wananchi kwa ujumla. Masomo hayo hufanyika kila siku, mara tatu kwa wiki na yanaendeshwa na waalimu mahiri wa kihindi.

Wanafunzi wanaoshiriki wanasema kwamba masomo huwasaidia kupumzika, kuimarisha ulinzi ya miili yao, huongeza wepesi, nguvu na stamina. Jinsi walivyozidi kuhudhuria wameweza kujenga kujiamini, nidhamu, kujitambua na uwazi.

Taasisi ya Sanaa ya Pharos

Sanaa Pharos ni taasisi iliyojikita katika elimu ya msingi yenye kukuza ari ya sanaa na ubinadamu. Taasisi hii inakaribisha wanamuziki na wasanii kutoka nje ya nchi, na hivyo kutoa uwezo kwa umma wa Cyprus nafasi ya kuona uzoefu kutoka kwa wenzao kimataifa, imekuwa ni kawaida kwa benki kutoa msaada kwa taasisi hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Paa la wazazi waliopekee Larnaca

Mnamo Desemba 2012 wafanyakazi wa Benki walipitisha msaada wa kusaidia familia tisa zilizokuwa zinakabiliwa na hali ngumu ya fedha. Katika familia hizo, kulikuwa na moja ambayo mzazi alikuwa mmoja akiwa na watoto wanne, alikuwa akiishi katika nyumba ambayo paa ilikuwa ikivuja na kufanya plaster za kuta kuanguka.

Wafanyakazi na uongozi wa Benki ulifanya ukusanyaji baina yao na walifanikiwa kuchanga kiasi cha € 6000 ambayo ilitosha gharama ya kujenga paa na vilevile kuwezesha familia kuishi katika hali nzuri; aidha wafanyakazi walitoa, nguo, samani, vifaa na chakula.

Yafuatayo ni mashirika ambayo yamepokea na kufaidika na misaada kutoka FBME

• Shule ya Evangelismos
• Chama cha Wazazi wa shule ya 4 Aglantzia Elementary
• Taasisi ya utamaduni ya Argaki
• N.V.C.
• Chama cha watoto wasioona Pancyprian
• Ubalozi wa Tanzania Moscow
• Kennedy Publications
• Limassol Phoenician Lions Club
• Ay. Nicolaos Gata Convent
• “Angels Live Among us”
• Kanisa la Othodoksi la Urusi
• Chama cha watu wasioona
• Europa Uomo
• Ziara ya Papa Cyprus
• Shule ya New Hope
• Xamogelo tis Zois
• Chama cha kimataifa cha Cyprus
• Chama cha Figo Cyprus
•Taasisi ya Aikionides
• Ecole Francaise
• Pharos Trust
• Taasisi ya sanaa Pharos
• Umoja wa michezo wa Viziwi
• Jumuiya ya kuzuia saratani Cyprus
• Chama cha watoto wenye mahitaji maalum
• American Academy
• Ilarchos
• Kituo cha Ushauri cha kiroho cha Mtakatifu wa Kykkos
• Center for Preventive Paediatrics
• Manispaa ya Nicosia
• Hospitali ya Askofu Mkuu Makarios III
• Make a Wish
• Shule ya awali ya umma Engomi
• Radiomarathonios
• Love the children day fund
• Cyprus Autism Association
• Familia za Armenia walioathirika na vita Syria
• Pasykaf
• Aglantzia Gymnasium
• Rotary Club ya Nicosia
• Shule ya kimataifa ya Marekani
• Maronite Archbishopric
• Ay. Varvara Church
• Chama cha waamuzi wa mpira wa kikapu
• Cyprus Foundation for muscular dystrophy research
• Shirikisho la Viziwi Cyprus
• Vestnik Kipra
• Ayios Mnasoni
• Shirika la matatizo ya figo Pancyprian
• Kyrenia Chrysocava Foundation
• Ladies Circle No 4
• Taasisi ya Kimataifa ya Usimamizi Cyprus
• Taasisi ya Kimataifa ya Biashara Cyprus
•Aidha kulikuwa na michangombalimbalikwa watu binafsi.

Pamoja na Amri ya kuifunga benki iliowekwa na Benki Kuu, juu ya FBME tawi la Cyprus, tarehe 21 Julai 2014, kulikuwa na mipango zaidi iliokuwa imepangwa.