Monthly Archives: Disemba 2015

Wenye Hatia Ni Nani?

Desemba 24, 2015

 Tangia Julai 2014, mwanzo wa sakata lake dhidi ya Benki ya FBME, Benki Kuu ya Cyprus (CBC) imewapeleka wadau kwenye mlolongo wa kushangaza wa vitendo visivyo na mantiki vilivyoibua maswali muhimu kuhusu uaminifu wake kama chombo cha serikali katika siasa za kisasa za Ulaya. Kwa kipindi kirefu cha miezi hii 17, CBC ilikuwa kimya kueleza nia yake, na ni hivi karibuni tu ndio wameanza kuonyesha ukweli wa yale yaliokuwa yakiendelea nyuma ya pazia, na hii ni dalili ya kushindwa kwenye vita vya kisheria kwenye midani ya kimataifa.

Continue reading

FBME Yapambana na CBC Kisheria dhidi ya Ubatilishaji wa Leseni Yake

21 Desemba 2015

FBME Limited imetangaza kuwa hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa kupinga kusitishwa kwa leseni, kulikofanywa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) dhidi ya Benki ya FBME Tawi la Cyprus, na uamuzi huu kwenye mahakama ya Cyprus.

Tamko la ubatilishaji huo lenye kurasa 9 limewasilishwa leo Desemba 21, 2015, ikilaumu watendaji wengine kwa vitendo vilivyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na Bodi ya CBC katika kipindi cha miezi 17, ambayo imetokana na CBC ilipofanya jaribio la uuzaji wa Benki ya FBME ya tawi Cyprus. FBME inapinga kabisa kubatilishwa kwa leseni hiyo.

Hatua hii ya kidhalimu ya CBC dhidi ya FBME, ambayo ni ya hivi karibuni, imesababisha kesi mbili nchini Cyprus na nje ya nchi, na kuziacha mamlaka za Cypruskwenye mlolongo wa madai ya uharibifu mkubwa na fidia.

Barua ya Wazi ya Alekos Markides kwa Rais

Desemba 15, 2015

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Cyprus, Alekos Markides ameandika barua ya wazi kwa Rais Nicos Anastasiades, akimuonya madhara kwa jinsi kesi ya Benki ya FBME inavyoshughulikiwa, pamoja na hatua kadhaa za kidhalimu zilizochukuliwa na Benki Kuu ya kisiwa cha Cyprus dhidi ya Benki. Matokeo ya hatua hizi yameivua nguo serikali ya Cyprus na walipa kodi wake kutokana na madai makubwa ya kuichafua hadhi ya Benki.

Kuona tafsiri ya barua ambayo Mheshimiwa Markides ameituma kwa niaba ya wamiliki wa Benki ya FBME, bofya hapa