Wanahisa Waonya Kuhusu Madai Yajayo

Agosti 19, 2014

Wanahisa wa FBME Benki watatumia kila upenyo kisheria uliopo, kwa kupinga uhalali wa Benki Kuu ya Cyprus kutoa mamlaka ya uuzaji wa tawi la Cyprus Hii ni kesi ya wazi ya Benki Kuu ya Cyprus kipitiliza mamlaka yake. Benki Kuu imepuuza ukaguzi wa hivi karibuni kuonyesha kwamba FBME Benki inakidhi mahitaji ya kupambana na pesa chafu kwa Benki Kuu ya Cyprus na Sheria zote muhimu za Ulaya. Uamuzi wa Benki Kuu ni wenye madhara si tu kwa Benki ya FBME lakini kwa sekta ya benki ya Cyprus kwa ujumla. Tunaamini kwamba uamuzi mbaya wa kutaka kuiuza Benki unaficha juhudi za wadau wengine za kutaka kuichukua benki tajiri na yenye fedha kuliko zote nchini Cyprus kwa kutumia nguvu za serikali. Tutatumia kila liwezekanalo kisheria kuzuia uuzaji huu na tunaweka ilani kwa mnunuzi yeyote kwamba anapaswa kuwa na ufahamu wa mazingira haya.