KUHUSU SISI

Hii ni tovuti kwa ajili ya FBME Limited, kampuni tanzu ya Benki ya FBME, Makao Makuu na matawi yake na ofisi ya uwakilishi za yakiwa Tanzania, Cyprus na Urusi. Tovuti hii imeanzishwa ili kukabiliana na kitendo cha Benki Kuu ya Cyprus kuchukua uendeshaji wa tawi la Cyprus la benki ya FBME.

Hatua hiyo ya  Benki Kuu imesababisha uzuiaji wa utoaji wa taarifa kwa umma pamoja na ushauri kwa wateja wa FBME na washirika wake, na hata ujumbe wa kutoa msaada na faraja kwa wafanyakazi wake. Kwa matokeo hayo, kampuni tanzu imetayarisha tovuti hii kama njia ya kutoa taarifa inayohisi ni muhimu kwa umma kuelewa.

Tulikotoka

Kitendo cha Benki Kuu ya Cyprus kuchukua udhibiti wa tawi la Cyprus la Benki ya FBME kilianza Julai 17, 2014 baada ya kutolewa taarifa ya matokeo ya utafiti wa FinCEN, Ofisi ya Marekani – Idara ya Hazina (tarehe 15 Julai).
Muhtasari wa kilichojiri na matukio na matukio ya baadae unaweza kuyapata kwenye tovuti hii chini ya kichwa: ‘Kilichotokea na Lini”, katika sehemu ya “Kuhusu sisi”.

Mara tu baada ya Benki ya FBME kusikia taarifa ya Marekani, ilitoa mwaliko kwa Benki Kuu ya Cyprus kusimamia shughuli ili kurejesha imani FBME. Hii ilikuwa siku ya Ijumaa tarehe 18 Julai. Kazi iliendelea kwa msingi huu hadi jioni ya Jumatatu Julai 21, majira ya saa 5 usiku, Benki Kuu ghafla ilitangaza amri kuchukua na kuuza tawi la Cyprus la Benki, hatua ambayo FBME Limited iliiona kama yenye uhasama na imepinga hatua hii katika mahakama.

Maamuzi haya ya haraka ya Benki Kuu ya Cyprus yalikuwa ni ya pupa na yenye nia mbaya.

Tangu Julai 21 Msimamizi Maalum, Dinos Christofides, aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus aliamua kuzuia miamala ya wawekaji fedha. Imedaiwa kuwa hii ni kutokana na kukosekana kwa benki mwambata, lakini hii si kweli.

Nchini Tanzania, makao makuu na matawi yanafanya kazi chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania. Hali iliyopo Tanzania ni tofauti kabisa na mdhibiti anaruhusu huduma za benki kuendelea kutolewa kwa wateja chini ya usimamizi wake. Ni wazi kuwa hali hii ilitakiwa itokee hata Cyprus.

Maoni ya umma

Kama sehemu ya utii kwa idara ya Hazina ya FinCEN Marekani, maoni ya umma yaliandaliwa na kampuni ya sheria ya kimataifa Hogan Lovells, ripoti hiyo ambayo inapatikana kwa kubonyeza hapa?

Taarifa ya FBME

FBME Limited ni kampuni tanzu ya benki ya FBME. Asili ya kampuni hii imeanzia miaka ya 1930 wakati Bwana Michel Saab alipokuwa mwakilishi wa kampuni ya ujenzi. Katika miaka ya mwanzo ya 1950 alianzisha Federal Benki ya Lebanon SAL (FBL)

Federal Benki ya Mashariki ya Kati Limited ilianzishwa nchini Cyprus mwaka 1982. Kutokana na masuala ya kibiashara ilisajiliwa katika Visiwa vya Cayman mwaka 1986 na kubadili jina lake kuwa FBME Limited mwaka 2005. FBME Benki Limited na Federal Benki ya Lebanon SAL hii leo ni vyombo viwili tofauti kabisa.

Mwaka 1982 FBME Benki Limited, tawi la Cyprus ilipewa leseni ya kuendesha biashara ya kibenki nchini Cyprus chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus, na kwa zaidi ya miaka 30 sasa FBME Benki Limited imekuwa ikifanya biashara nchini Cyprus.

Benki iliandikishwa tena nchini Tanzania mwaka 2003 sambamba na mkakati wa FBME katika masoko ya nchi zinazoendelea na hususan fursa maalum ya kibiashara iliyojitokeza kwa kukubali baadhi ya mali na madeni ya benki nchini Tanzania ambayo ilikuwa na leseni kamili ya benki. Benki inaendelea kufanya kazi zake chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania.

Umiliki wa awali ulikuwa kati ya mwanzilishi, Bw Michel Saab na wanawe, ila baadaa ya kifo cha Bw Michel mwaka 1991, FBME Limited imekuwa inamilikiwa kwa hisa sawa baina ya Bw Ayoub-Farid M Saab na Bw Fadi M Saab.

Kupitia kampuni tanzu na vitengo vyake, watu 438 wameajiriwa nchini Cyprus, Tanzania na Urusi, kati ya hao 200 ni raia wa Jamhuri ya Cyprus. Wateja wa benki hii wakitokea maeneo tofauti ya kijiografia kutoka nchi zinazokaribia 50 duniani.

Ni nini kilichotokea na Lini – Chanzo cha Suala hili Imesasishwa Septemba 1, 2014

FBME Limited inaweka wazi hapa chanzo na maendeleo kuhusu ‘Tangazo la matokeo ya Uchunguzi’ pamoja na Ilani ya ‘Hatua za Kuchukuliwa’ iliyotolewa na ofisi ya FinCEN, Idara ya Hazina ya Marekani, na maamuzi ya baadae yaliyochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus na msimamizi wake Maalum kuhusiana na tawi la Cyprus la Benki ya FBME
• Julai 15, 2014 FinCEN, Ofisi ya Idara ya Hazina ya Marekani, ilitoa ilani ya hatua za kuchukuliwa baada ya kuitaja FBME kama taasisi ya fedha ya kigeni “Inayotakatisha Fedha Chafu’ kwa mujibu wa kifungu 311 cha USA Patriot Act” na hivyo kutoa Tangazo la matokeo ya Uchunguzi. Hii ilitolewa kwa umma tarehe 17 Julai.

• Mara baada ya FBME kufahamu uwepo wa tangazo hilo, ilichukua hatua za haraka na tarehe 18 Julai kampuni tanzu ilishirikisha washauri wake wa kisheria wa muda mrefu, Hogan Lovells, kuwakilisha maslahi yake kwa Idara ya Hazina ya Marekani na kuwaeleza msimamo wa Benki kutoa ushirikiano wa kutosha.

• Asubuhi ya Julai 18, 2014 Benki iliomba kufanya mkutano na Benki Kuu ya Cyprus na kuwaalika kuja kusimamia shughuli za benki ili kurejesha imani kuwa taratibu za Kupambana na Fedha chafu zinafuatwa hususan na Mabenki waambata.

• Julai 18, 2014, baada ya mwaliko kutoka kwa wanahisa wa FBME, Benki Kuu ilitangaza kuchukua usimamizi wote wa FBME benki ya Cyprus chini ya sheria husika. Malipo ya nje yalisitishwa.

• Wakati huo, uwezo Kifedha wa Muda mfupi wa Benki ulikuwa na uwiani wa asilimia 104, ikiwa na maana kwamba inauwezo wa kuwalipa wateja wote.

• Ilipofika saa 5 usiku tarehe 21 Julai, baada ya siku moja tu ya usimamizi wa kudhibiti, Benki Kuu ya Cyprus iliyotoa Amri ya uuzaji wa tawi la FBME katika Jamhuri ya Cyprus na wakati huo huo kuwasilisha taarifa hizo kwa Wanahisa wa FBME Benki.
FBME inaona huu ni uvamizi na hivyo kuchukua hatua za kimahakama kuzuia chini Cyprus. Ilikuwa ni njama za hasama na za pupa kwa maamuzi hayo kuchukuliwa, ukizingatia kipindi hicho kifupi.

• Mnamo tarehe 21 Julai wanasheria wa Benki waliopo Marekani walionyesha kuwa Idara ya Hazina ya Marekani ilionyesha nia ya kuingia katika mazungumzo na Benki na kupokea maelezo ya ziada kutoka Benki yanayo husu suala hilo.

• Kipindi cha siku nne za kazi 23, 24, 25 na 28 Julai zilizofuata, tawi la Benki la Cyprus lilifungwa na wateja wake kuzuiwa kupata huduma ya kifedha.

• Kutoka Julai 29 malipo machache yalirejeshwa baada ya kupitishwa na msimamizi aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus. Hata hivyo, kikawaida idhini ya malipo ilikuwa ndogo au kukataliwa. Benki Kuu inasema hii ni kutokana na kukosekana na benki mwambata, sababu ambayo sio ya kweli.

• 30 Julai, Wanasheria kutoka Hogan Lovells na wakaguzi wa Ernst and Young, kutoka marekani, waliwasili Cyprus kwa lengo la kuisaidia FBME na Wanahisa wake katika kufikia utatuzi wa masuala yaliyotolewa na taarifa FinCEN. Awali walikataliwa kuingia ofisi za FBME na msimamizi Maalum, hii ilitenguliwa na ushauri wa mahakama za Cyprus.

• Julai mwishoni Mahakama Kuu ilianza kulisikiliza shauri la wanahisa wa Benki kuhusu zuio la uuzaji wa tawi la Cyprus na shauri hili lilipangiwa tarehe 7 Agosti. Uamuzi wa mahakama siku iliyofuata haukukubaliana na zuio na hivyo kutoa fursa nyingine za kisheria kulizinduliwa.

• Kitengo cha huduma za kadi cha FBME kilisimamisha huduma za kibiashara tarehe 7 Agosti, ikifuatiwa siku tano baadaye na tangazo la kupunguzwa kwa wafanyakazi. Wafanyakazi wapatao 72 walipunguzwa kazini na wengine watatu kupewa notisi ya kupunguzwa wakati wowote. Wafanyakazi wote walielezwa na watapokea stahili zao kamili. Uamuzi huu wa kusikitisha umekuja kutokana na matendo Msimamizi Maalum ya kuzuia miamala. Kwa sasa Cyprus imeachwa na ukiritimba wa mtoaji mmoja tu kadi.

• Usajili katika usuluhishi na Chemba ya Kimataifa ya Biashara ya Paris, kutaja haki za mwekezaji chini ya mkataba wa makubaliano baina ya Lebanon na Cyprus tangu mwaka 2002, uliwasilishwa kwa Msimamizi Maalum tarehe 14 Agosti.

• Stefaan De Rynck, Mkuu wa Kitengo cha Tume ya Ulaya Kurugenzi ya masoko ya Ndani na Huduma, aliwaandikia wanasheria wa FBME kwamba Tume hiyo itafuatilia kwa makini hali ya Cyprus ili kuhakikisha kuwa hakuna sheria za EU zitakazovunjwa.

• Tarehe 19 Agosti, Fitch Ratings ilitoa ripoti kuonyesha wasiwasi wake kwa matumizi ya hatua na maazimio juu ya tawi la benki ya kigeni. Majibu rasmi ya shukrani kutoka kwa wanahisa yalitolewa kwa kampuni hiyo kuhusu maoni yake juu ya jambo hili.

• Benki Kuu ya Tanzania ilidhihirisha nafasi yake katika kesi benki ya FBME, ikiongeza kuwa hakuna maelekezo yatakayotendeka bila ridhaa yake katika masuala yanayohusiana na Benki.

• Mahakama Kuu ya Cyprus ilitoa maelekezo tarehe 22 Agosti kutaka majadiliano zaidi kuhusu uuzaji wa FBME tawi la Cyprus yasifanyike hadi 15 Septemba, na Benki Kuu ya Cyprus ilitoa ahadi ya kutoendeleza na uuzaji mpaka tarehe hiyo.

• Barua ilitumwa tarehe 26 Agosti kwa wafanyakazi wa FBME Benki kutoka kwa mmiliki mwenza Fadi M Saab kutoa shukrani kwa wafanyakazi kwa uaminifu wao katika nyakati hizi ngumu na kuonyesha mkakati wa kushughulika masuala yanayoikabili Benki.

• Wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa madhara kwa FBME Benki, wamiliki wakatangaza nia yao kuwashughulikia binafsi watu ambao watathibitika kuhusika na jambo hili na kuwawajibisha.

• Benki Kuu ya Cyprus yatoa taarifa Agosti 28, na kusema kwamba haina uadui na Benki ya FBME, ambayo ilifurahiwa na wamiliki wake. Hii ni mara ya kwanza kujieleza kwa umma kwa Benki Kuu au Msimamizi kwa wiki kadhaa.

• Msimamizi alitoa taarifa Septemba 1, kupitia tawi la benki la Cyprus, kuwa wateja wataweza kufanya miamala hadi Euro 10,00 kwa siku. FBME Limited ililikaribisha wazo hili kwa furaha ingawa baadaye ilibainisha kuwa utekelezaji wake ulikuwa wa kutoridhisha na pia kuwa na vikwazo vingi, na ilifanyika bila ya kuwapa taarifa Mdhibiti wa makao makuu nchini Tanzania.

  • Masuala yanayoibuka kutokana na dhamira ya Msimamizi ni kuruhusu wateja kuweza chukua fedha zao, kiasi cha hadi EUR 10,000 kwa siku. Kikwazo kilichopo ni kwamba upatikanaji wa hichi kiasi ni kwa wale wateja waliopo Cyprus. Hii ni kwa sababu ameruhusu shughuli hizi kufanywa katika tawi moja tu la Benki ya Cyprus, ambapo wateja hulazimika kufungua akaunti na taasisi hii. Idadi kubwa ya akaunti za wateja hubaki zimehifadhiwa, kitu ambacho husababisha taratibu zisizo sawa kwa wateja waliolingana
  • Kwenye tarehe 5 Septemba tovuti hii ya fbmeltd.com iilikuwa haipatikani kutokana na kile tulichoambiwa kuwa wimbi kubwa kwa walengwa kunyimwa huduma “kutokana na “udukuzi”. Kitendo cha haraka kilichukuliwa kuihamisha tovuti nje ya Cyprus na ndani ya masaa 24 huduma ya kawaida iliweza kupatikana tena
  •  Maelezo yalibainishwa wazi kuhusu kusimamishwa shughuli katika kitengo cha FBME Kadi, na Msimamizi alitambuliwa kuwa ndio jukumu lake katika kuwasimamisha watu 75 kazi. Alidai chanzo kilikuwa ni ukosefu wa fedha kutokana na kuanguka kwa mipango ya mawasiliano ya benki , wakati huo huo Benki Kuu ya Cyprus bado ilikuwa ikishikilia EUR milioni 100 ya FBME Bank kama amana. Ieleweke kuwa EUR milioni 2 ingeweza kutosha kuiweka kitengo hicho cha Kadi katika utendaji.
  •  Baada ya kubainisha na uchapishwaji wa taarifa hizo za ufungwaji wa kitengo cha Kadi, Msimamizi alitoa majibu ya hasira kwamba asingepitisha malipo kwa ajili ya kitengo hicho. Vitisho hivi havijabatilishwa.
  • Kushindwa kwa Jamhuri ya Cyprus kuwasilisha faili kwa wakati katika Mahakama ya Wilaya ya Nicosia umesababisha mahakama kuahirisha maamuzi kutoka Septemba 15 hadi Septemba 29, tarehe ambayo maelekezo yangefanywa kuhusu ombi ya muda mfupi yaliowasilishwa na wanahisa wa FBME.
  •  Tarehe 18 Septemba taarifa juu ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus na msimamizi wake zilichapishwa. Suala hili na maswali yalioelekezwa kwa mamlaka hayajajibiwa.
  •  Wanasheria wa kimataifa Hogan Lovells, waliwasilisha mrejesho wa madai kwa FinCEN kwa niaba ya FBME Bank Limited na, mrejesho huo ulibainisha uchunguzi wa kina uliofanywa na wahasibu wataalamu wa kuchunguza EY (Ernst and Young).   Waraka huo wa kurasa 28 uliotolewa na Hogan Lovells tarehe 22 Septemba, unapatikana kwenye tovuti hii, fbmelimited.
  •  FBME imedhihirisha kuwa inafuata kanuni na imeonyesha dhamira yake ya kushirikiana bega kwa bega na na wakuu wake. Katika kuweka wazi matukio yaliojiri, FBME imeomba kwa heshima zote, mapendekezo yaliotolewa kwenye ilani iliotolewa FinCEN yaondolewe.
  •  Tarehe 29 Septemba, katika kikao cha Mahakama ya Wilaya(baada ya kucheleweshwa kutoka 15) kesi ilisikia maombi ya wanahisa wa FBME yaliowasiliwishwa dhidi ya uuzaji wa tawi la Cyprus na ikapangwa tena tarehe 21 Oktoba.
  • Wanahisa wa FBME wametangaza kwamba mshauri wake wa kisheria katika usuluhishi wa ICC ni Quinn Emanuel, msuluhishi aliyeteuliwa ni Profesa Ibrahim Fadlallah, mtaalamu anayeongoza katika masuala ya sheria na Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Paris.
  • Desemba 5 ilikuwa siku ya mwisho kwa Jamhuri ya Cyprus kuwasilisha majibu ICC na maelezo ya msuluhishi wake. Jamhuri iliomba iongezewe muda ambapo ilipewa hadi Januari 7.
  • Wanahisa wa FBME wametangaza kwamba mshauri wake wa kisheria katika usuluhishi wa ICC ni Quinn Emanuel, msuluhishi aliyeteuliwa ni Profesa Ibrahim Fadlallah, mtaalamu anayeongoza katika masuala ya sheria na Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Paris. Desemba 5 ilikuwa siku ya mwisho kwa Jamhuri ya Cyprus kuwasilisha majibu ICC na maelezo ya msuluhishi wake. Jamhuri iliomba iongezewe muda ambapo ilipewa hadi Januari 7.
  • Imejulikana kwamba Benki Kuu ya Cyprus inaitoza Benki ya FBME tozo ya adhabu ya mamlaka ya Benki za Ulaya ECB-juu ya fedha za ziada zilizopo kwenye akaunti ya FBME. Hii ni licha ya kuwekwa mazingira ambapo FBME amelazimika kuweka fedha hizo ndani ya Benki Kuu. Msimamizi ameihakikishia FBME kwamba adhabu hii itaondolewa.
  • Imejulikana kwamba Benki Kuu ya Cyprus inaitoza Benki ya FBME tozo ya adhabu ya mamlaka ya Benki za Ulaya ECB-juu ya fedha za ziada zilizopo kwenye akaunti ya FBME. Hii ni licha ya kuwekwa mazingira ambapo FBME amelazimika kuweka fedha hizo ndani ya Benki Kuu. Msimamizi ameihakikishia FBME kwamba adhabu hii itaondolewa.
  • Desemba 10-15, Msimamizi ajipa likizo isiyoelezeka kutoka Tawi la Benki ya FBME la Cyprus, hivyo kulazimisha kufunga shughuli za miamala. Taarifa ya masaa machache tu ndiyo iliyotolewa.
    • Katika kulikataa ombi la muda la Wanahisa la kuzuia mapendekezo yoyote ya uuzaji wa Tawi la Benki ya FBME Cyprus, kitendo kilichoonekana kama cha uvamizi, tarehe 17 Desemba Mahakama ya Wilaya ya Nicosia ilipuuza ombi la Wanahisa wa FBME la kufungua jalada kwa ajili ya usuluhishi. Wanahisa wamekata rufaa.
    • Kiwango cha kila siku cha Msimamizi wa Benki Kuu kuidhinisha miamala kwa wateja wa FBME kimepunguzwa hadi kufikia EUR 1,000 kutoka EUR 2,000. Sababu inayotolewa ni ‘wasiwasi juu ya ukwasi’ licha ya ukweli kwamba Benki Kuu ya Cyprus ina fedha nyingi zaidi za FBME kuliko wakati mwingine wowote kinachofikia EUR 155,000,000.

  • Januari 21, FinCEN yafanya mkutano na wawakilishi wa Benki ya FBME jijini Washington kutathmini majibu ya madai yake ya awali dhidi ya Benki yaliyofanywa Julai 2014. Benki ya FBME , kwa heshima kubwa imeiomba FinCEN kuondoa ilani ya NPRM na kuahidi ushirikiano zaidi na FinCEN.
  • Jopo la watu watatu wa mahakama linaundwa na Profesa Pierre Tercier (mwenyekiti), Profesa Ibrahim Fadlallah na VV Veeder QC. Moja ya kazi yake ya kwanza ni kuangalia madhara yaliyofanywa dhidi ya Benki ya FBME tangu Oktoba 28 wakati shauri la usuluhishi lilipofunguliwa.