Kauli kuhusu Hotuba kwenye Bunge la Tanzania iliyoihusu FBME Bank Ltd

21 Juni, 2021

“Tunafahamu kuhusu kauli ya hivi karibuni (FBME Bank resurfaces in Parliament over payments – The Citizen)   kwenye Bunge la Tanzania ya mbunge mkongwe wa Bunge hilo, kuhusu kuendelea kushindwa kwa Benki Kuu (BOT) na Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kuwezesha amana zilizopo kwenye benki ya FBME kufikiwa na kulipwa kwa wenye amana tangu benki hiyo ilipowekwa chini ya usimamizi.

Ifahamike kuwa benki ya FBME ilikuwa na ukwasi wa kutosha na uwezo wa kuwalipa wateja wake ndani ya Tanzania na pia kwenye tawi lake nchini Cyprus kabla haijawekwa chini ya usimamizi.

Tunapenda kuelezea masikitiko yetu kwamba mwenye amana na waliokuwa wafanyakazi wa benki ya FBME wameendelea kutopokea ushirikiano kutoka Benki Kuu na Bodi ya Bima ya Amana, na kwamba baadhi ya wenye amana wamefariki dunia tangu benki hii ilipowekwa kwenye usimamizi bila hata kupata amana zao zilizokuwa benki. Hili ni Janga!

Sisi kina Saabs mara zote tumekuwa tayari kusaidia (na tumekuwa tukiomba fursa hiyo) katika kuipatia utatuzi hali hii kwa wateja/wenye amana, waliokuwa wafanyakazi na wadai pia”