Monthly Archives: Machi 2015

Amri ya EUR 200 kwa siku yaleta matatizo kwenye mishahara ya wafanyakazi

Machi 20, 2015

 Kuna ushahidi mkubwa wa matatizo yanayowakabili na watu wanaofanyia kazi makampuni yaliowekewa vikwazo ya utoaji wa EUR 200 kutoka akaunti zao FBME Cyprus. Kiwango hicho chenye ngazi ya EUR 200 kimekuwepo kwa ajili ya mashirika pamoja na watu binafsi tangu mwanzo wa mwezi Machi katika hatua ya kibabe iliyotungwa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus. Awali ilikuwa EUR 1,000 kwa siku.

Continue reading

Ripoti za waandishi: Barua kutoka Wanasheria kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Machi 20, 2015

 Kuna ripoti inayonekana kwenye tovuti ya chombo cha habari kinacho ongoza vyombo vya habari, Sigmalive, ambayo inahusu barua iliyoandikwa na mshauri wa kisheria wa nje wa FBME na imepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri. Yaliyomo ni malalamiko ya nguvu yakielekezwa kwa Dinos Christofides kuhusiana na jukumu lake kama msimamizi aliyeteuliwa kuendesha tawi FBME Benk, pamoja na mashtaka ya kwamba inawezekana kuwa wamevunja sheria.

Continue reading

Wapili ajiuzulu kutoka Bodi ya CBC

Machi 20, 2015

 Stavros Zenios, mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Cyprus, alijiuzulu kutoka Bodi asubuhi hii ya Machi 20. Yeye ni mwanachama wa pili kuachia nafasi hizo katika siku za karibuni, Stelios Kiliaris alijiuzulu wiki iliyopita akitoa maelezo kuwa haiwezekani kuendelea kutumikia mamlaka hiyo katika mazingira ya sasa. Bw Kiliaris pia alikuwa mmoja kati ya wanachama watatu wa kamati walioiwekea FBME azimio la masharti.

Continue reading

Sera Potofu Za Mamlaka ya Azimio

Machi 12, 2015

 Makala hii inafuatia kutoka hapo juu, Mamlaka ya Azimio Yaelea Kwenye Bahari ya Matatizo.

Mamlaka ya Azimio ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) – ambayo kiukweli ni Bodi yake ya Wakurugenzi – na Kamati ya Azimio – wajumbe watatu wa Bodi hiyo – wanaonekana, bila shaka, wanawajibika kwao wenyewe na si kwa mwingine. Walivurunda kwenye Azimio la Benki ya Laiki iliyopo hapa kisiwani, na kusababisha matatizo makubwa nchini kote na wametumia tafsiri potofu ya Azimio la Amri na kulipoka tawi la Benki ya FBME. Katika mchakato huo, wamesababisha kutoaminiwa kwa kiasi kikubwa kwa Benki Kuu, kuharibu fursa ya kulinda wamiliki wa akaunti na wadai, na kuhatarisha malipo ya fidia kwa mamia ya mamilioni ya Euro.

Continue reading

Mamlaka ya Azimio Yaelea Kwenye Bahari ya Matatizo

Machi 12, 2015

   Tafakari juu ya kazi ya Mamlaka ya na Kamati ya Azimio ya Cyprus.

Mamlaka ya Azimio na Kamati ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) wanaandamwa na vyombo vya habari kwa wakati huu, na hakuna hata chombo kimoja kilicho kwenye upande wake. Linalozungumzswa sasa ni kuhusu Utawala wa benki iliyofungwa ya Laiki, ambapo wamiliki wake wa akaunti wa Cyprus wamepata hasara kubwa ya mamia ya mamilioni ya Euro. Linaloleta mgogoro kwa sasa ni kuhusu hatua ya kisheria ya Mamlaka ya Azimio dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Benki ya Laiki, Andreas Vgenopoulos. Msimamizi iliyeteuliwa kushughulikia Azimio la Laiki, Andri Antoniades, alijiuzulu Jumatatu Machi 2, na kuwalaumu Gavana wa Benki Kuu na Mamlaka ya Azimio kwa masuala ya kijinga yanayohusishwa na kesi za kisheria, ikiwa ni pamoja madai kwamba binti wa Gavana bado analipwa mshahara na Mwenyekiti wa zamani wa Laiki pamoja na ahadi zilizotolewa mapema kuwa angejiuzulu.  Continue reading

Maamuzi ya Kutapatapa huku CBC Ikielekea kukwama

Machi 13, 2015

 Pamoja na kukabiliwa na matatizo lukuji waliojisababishia wenyewe Benki Kuu ya Cyprus (CBC) inajitutumua na maamuzi mabovu zaidi na kuthibitisha kuwa wao bado ni chombo hatari wakati Gavana na Wakurugenzi Waandamizi wa CBC, (mmoja amejiuzulu jana) wanakabiliwa na maswali toka kwa wabunge na pia matatizo la malipo ya fidia yakiendelea kukua siku hadi siku, CBC inajali tu kuendeleza upuuzi wake.

Continue reading

CBC Waruka Kadri Ukweli Unavyojiri

Machi 15, 2015

 Habari zilizofika FBME ni kwamba Jamhuri ya Cyprus katika Mahakama ya Usuluhishi ya ICC mjini Paris, inataka tawi la Benki ya FBME Cyprus lifungwe kwa misingi kwamba hakuna wanunuzi waliopatikana kununua tawi hilo. Kwa maneno mengine, kwa sababu azimio lililotolewa kwa kulazimisha na Benki Kuu ya Cyprus Julai mwaka jana halikufanikiwa kwa hiyo wanataka kunyang’anya leseni ya FBME. Wanaongeza ya kwamba wanataka kufanya hili sasa kwa sababu kufungwa kwake kutawezesha ulinzi wa bima ya amana kutumika na fedha za FBME zinazoshikiliwa na CBC (EUR 158,000,000) zitaweza kutumika kufanya malipo hayo.

Continue reading

Benki Kuu ya Cyprus yaiondolea FBME adhabu

Februari 27, 2015

Kwa niaba ya wote wanaohusiana na Benki ya FBME, tovuti hii inaishukuru Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na Msimamizi wake kwa kusimamisha tozo ya adhabu kwa FBME kwa kuwa na kiwango cha juu cha fedha kuliko kinachotakiwa na CBC. Mbali na kusitisha tozo hiyo, CBC pia imerudisha fedha ya adhabu iliyoichukua katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Wamefanya kazi nzuri.

Continue reading