Monthly Archives: Mei 2016

Uamuzi wa Mahakama ya Utawala Waonekana Kutokuwa Sahihi

Mei 27, 2016

Maamuzi ya Mahakama ya Kiutawala ya Cyprus kukataa maombi ya Benki ya FBME kuahirisha hatua iliyopangwa ya Benki Kuu ya Cyprus ya kufuta leseni ya tawi ka FBME imetangazwa kuwa hayana mashiko. Maombi ya awali yalifanywa takriban miezi 21 iliyopita kwenye Mahakama Kuu ya Cyprus, na yalikuwa ni maombi kwa ajili ya hukumu ya mpito. Mahakama ya Utawala iliisikiliza kesi hiyo ili kupunguza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama Kuu, na inajulikana kwamba Mahakama ya Utawala haina kawaida ya kutoa maamuzi ya mpito.

Continue reading

Ombi la CBC la Kutaka Maelezo Binafsi ni Kinyume cha Sheria

Mei 24, 2016

Mawasiliano ya hivi karibuni kutoka Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kwenda kwa wamiliki wa akaunti wa tawi la Benki ya FBME Cyprus ni kinyume cha sheria na inapingana na maamuzi yoyote ya kisheria ya huko nyuma, FBME imesema. Mawasiliano hayo, yaliyoitwa na CBC “maelezo ya mwenye akaunti ‘”, yanawataka wamiliki wa akaunti kuwasilisha maelezo yao binafsi na ni mbinu ya mlango wa nyuma ya kuwafanya waombe malipo ya dhamana ya amana bila ya wao kujua.

Continue reading

Mkuu wa FinCEN Ajiuzulu

2 May 2016

Imetangazwa kwamba mkuu wa Idara ya Hazina ya Marekani FinCEN, Jennifer Shasky Calvery anaondoka kwenye idara hiyo. Kutokana na maelezo ya FinCEN, siku yake ya mwisho itakuwa 27 Mai, 2016.

Alijiunga na FinCEN mwaka 2012 na ameiongoza idara hiyo kwenye matatizo ya hivi karibuni ya kuyashambulia mabenki ikiwamo Benki ya FBME, kwa madai kuwa yana mifumo dhaifu ya kupambana na fedha chafu. Madai haya dhidi ya Benki ya FBME yamefunguliwa mashataka kwenye mahakama ya Maerkani.

Inasemekana Bi shasky Calvery anatarajia kujiunga na benki ya HSBC.