Monthly Archives: Disemba 2016

Mahakama ya Sheria Cyprus Yaruhusu Wanasheria wa FBME Kupatiwa Nyaraka Muhimu

4 Desemba 2016

Mnamo Novemba 29, 2016 Mahakama ya Utawala ya Cyprus, inayosikiliza kesi ya FBME dhidi ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC), imeiagiza CBC, kama Mamlaka ya Azimio ya Nchi, na Kamati Azimio, kuwaruhusu wanasheria wa Benki ya FBME kupata nyaraka muhimu kuhusiana na kuchukuliwa kwa Benki ya FBME tawi la Cyprus na CBC mwezi Julai 2014.

CBC imepewa siku saba kutekeleza agizo hilo.

Amri hiyo, ambayo inaonyesha hatua muhimu ya kesi hiyo ya kisheria, inaipa timu ya wanasheria ya FBME fursa ya kufanya mapitio ya mawasiliano, ripoti na nyaraka nyingine kuhusiana na kesi hiyo.

Hii ni sehemu ya muendelezo wa hatua za kisheria kuhusiana na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya FBME mwaka 2014 na baadae.

Kesi katika mahakama ya Cyprus, Mahakama ya Usuluhishi ICC mjini Paris, na hatua za kisheria nchini Marekani zinaendelea.