Monthly Archives: Disemba 2014

Mahesabu yaelezewa

                                               Desemba 12, 2014

Kama ilivyvotajwa katika toleo la tarehe 20 Novemba kwenye tovuti hii, Ukwasi mpya, makosa yanazidi kujitokeza ambapo faini inatozwa kwa malipo ya amana za wateja wa FBME Bank kwa amana ambazo zinahitajika zilipwe na Benki Kuu ya Cyprus kwa sababu ya matendo ya Benki Kuu yenyewe . Kwa maneno mengine, Benki Kuu imeagiza FBME kufanya kitu, na baada ya hapo inaipa adhabu ya ushuru kwa kufuata agizo hilo!

Continue reading

Arudia Tena!

Desemba 12, 2014

Je, hakuna mwisho wa kutowajibika na kiburi cha Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus? Amerudia kwa mara nyingine hila yake ya miezi michache iliyopita, na ametoweka bila kutarajiwa, kwenda kwenye mapumziko yasiyoidhinishwa. Kwa mara nyingine tena ameondoka bila kuacha mtu kwenye nafasi yake wa kuidhinisha malipo au mambo mengine yanayohusiana na tawi, na hakutoa tarehe ya kurudi. Hii imesababisha tawi kufunga shughuli zake na kuleta matatizo makubwa kwa wateja na wafanyakazi.

Continue reading

Msimamizi Arudi

Desemba 15, 2014

Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus, mwenye wajibu wa kuendesha Benki ya FBME tawi la Cyprus, amerejea leo baada ya kukosekana kusikoelezeka. Kama inavyojulikana, aliondoka saa 7 mchana siku ya Jumanne, na hivyo kuzuia muamala wowote kufanyika kwa wiki nzima. Matokeo haya ni kutokana na hatua ya kibabe inayomwezesha kuidhinisha miamala yote na kukataa kwake kuteua naibu kufanya kazi kwa niaba yake.

Hata hivyo, amesharudi na miamala ya kiwango cha EUR 2,000 kwa siku kwa kutumia hundi – uamuzi mwingine  wa kibabe – imeanza.

Ripoti Ya Uchunguzi Yawasilishwa

Desemba 3, 2014

  Desemba 1, 2014 Benki ya FBME imewasilisha kwa FinCEN ripoti ya uchunguzi yenye maelezo ya kina iliyotayarishwa na wataalamu kutoka kampuni ya ushauri ya kimataifa E & Y (Ernst & Young). Aidha, Benki imewasilisha kwa FinCEN mamia ya kurasa za nyaraka kuhusu programu yake ya kupambana na fedha chafu na taratibu zake za ‘Jua Mteja Wako’ (KYC). Uwasilishaji huo kwa FinCEN ulifanywa na kampuni ya kimataifa ya sheria ya Hogan Lovells kwa niaba ya Benki ya FBME.  Continue reading

Mahakama ya Wilaya ya Nicosia Yasitisha Hukumu

Desemba 2, 2014

 Jaji katika Mahakama ya Wilaya amesitisha hukumu kufuatia hati ya ziada ya wanahisa wa FBME tarehe 1 Desemba, baada ya kusikiliza maelezo ya mdomo na ya maandishi kuhusu kufungua jalada kwenye mahakama ya usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara mjini Paris. Kama ilivyo kawaida ya taratibu za kimahakama, amesitisha hukumu hadi tarehe ya baadae juu ya maombi ya muda mfupi ya wanahisa kuzuia uuzaji wa amana za tawi la FBME la Cyprus na kuzuia hatua za Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus zenye kuharibu zaidi biashara ya Benki hiyo.

 

Wanahisa Wadai Dola Milioni 500 kama Gharama ya Uharibifu

Novemba 28, 2014

 

Hati ya Usuluhishi katika kesi iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) na wamiliki wa FBME Limited, kampuni tanzu  ya Benki ya FBME, inaonyesha kwamba madai ya madhara dhidi ya Jamhuri ya Cyprus yanakadiriwa kufikia Dola za Kimarekani nusu bilioni kwa sasa.. “lakini kuna uwezekano wa kuzidi kiasi hiki wakati kesi ya  usuluhishi itakapokamilika.” ICC ina mamlaka ya mwisho ya kuamua  juu ya madai ya gharama za uharibifu huu. Nakala ya muhtasari wa hati ya usuluhishi inapatikana hapaContinue reading