Machi 1, 2022
Mahakama ya Utawala ya Cyprus ilitoa uamuzi wao kuhusu dai lililowasilishwa tarehe 24 Julai 2014 la kupinga hatua ya azimio hilo. Kwa ufupi, Mahakama ya Utawala ya Cyprus imeamua kwamba kwa muda wa miaka saba na nusu iliyopita Benki Kuu ya Cyprus imekuwa ikifanya kazi za kutoa maamuzi yote na uendeshaji wa Tawi hilo kinyume cha sheria`
Katika tarehe ya azimio Benki ya FBME Limited ilikuwa na fedha za kutoshaleza kuwalipa wenye amana wote kwa ukamilifu na ziada ikabaki kulipwa kwa Wanahisa, ambao kisheria wanasimama wa mwisho katika safu ya wadai.
Wanahisa waliwasilisha kwa uwazi uvunjwaji wa kisheria za kibiashara na msimamo wa Benki Kuu ya Cyprus tangu mwanzo lakini ulipuuzwa na hatimaye hawakuwa na chaguo jingine bali ni kuchukua hatua za kisheria.
Tangu 2014 Wanahisa walitafuta kuwalinda wenye amana na FBME Bank Limited. Wanahisa walishikilia kwamba Benki Kuu ya Cyprus inafanya kazi kinyume cha sheria lakini, hata hivyo, Wanahisa mara kwa mara waliitaka Benki Kuu ya Cyprus kushirikiana na wenye amana, Benki Kuu ya Tanzania ( Ambayo ndio Makao Makuu ya Benki ya FBME), na wanahisa kufanya kazi kwa pamoja ili kumaliza tatizo kwa haraka.
Badala ya kushirikiana na washikadau wote husika, Benki Kuu ya Cyprus iliendelea na vitendo vyake kinyume na sheria walitumia fedha za wenye amana na za benki kulipia gharama za mawakili, washauri n.k. katika kutafuta sababu za kuendeleza hali hiyo na kuhalalisha matumizi ya Benki kuu ya Cyprus hatua zisizo halali.
Tunaelewa, lakini bado hatujathibitisha rasmi, kwamba Benki Kuu ya Cyprus imemwondoa msimamizi wa sasa kutoka FBME Bank Limited tarehe 1 Machi 2022.
Wanahisa wanaitaka Benki Kuu ya Cyprus kukubali maamuzi yote ya mahakama za Cyprus, na kuwajibika kwa kipindi chote cha miaka saba na nusu iliyopita ya usimamizi mbaya usio halali ambao walioufanya, na kushirikiana na washikadau wote kukomesha mmomonyoko wowote wa fedha wa kulipa wote. wenye amana.
Wanahisa wanapendekeza mkutano katika ofisi za wanasheria wetu wiki hii ili kuanzisha mazungumzo yenye kujenga.