Msimamizi Aondoka Tena

Februari 18, 2015

Kama baadhi ya matukio ya mwaka 2014, Msimamizi ameondoka kwenda kwenye mapumziko yasioelezeka tangu Februari 18 hadi, inasemekana, Jumanne ijayo tarehe 24. Kama mwanzo, hajamteua yeyote kukaimu nafasi yake, hivyo kwa muda wote huo tawi la FBME la Cyprus halitoweza kutoa hundi.

Bila shaka, ni busara kabisa kwa Msimamizi kupata nafasi ya kupumzika mara kwa mara, sisi sote tunahitaji hilo. Hata hivyo, haihitaji busara kubwa kumteua mtu kushika nafasi yake ili kuidhinisha miamala.