Machi 4, 2015
Kama kuna sababu yoyote tangu mwanzo ya Benki Kuu ya Cyprus kumteua Dinos Christofides kama Msimamizi wa masuala ya Benki ya FBME tawi la Cyprus, kwa sasa inawasababishia kuonekana kama kinyago. Na bila shaka, kuna uwezakano wa kuwepo njama zinazoandaliwa dhidi ya FBME.
Kuanzia wiki hii, Msimamizi ameagiza kwamba kiwango cha muamala ambacho wamiliki wa akaunti wa Benki ya FBME (wanaoweza kufika Nicosia – Mji mkuu wa Cyprus) wanaweza kupata kimepunguzwa kutoka kiasi cha Euro 1000 hadi kufikia Euro 200 kwa siku. Sababu aliyoitoa anaandika:
“Hatua hii imechukuliwa kutokana na upungufu wa upatikanaji wa ukwasi nchini Cyprus na kukataa kwa mabenki waambata (Correspondence Banks) kurudisha fedha zetu zilizowekwa kwao,”
Inastaajabisha! Kiwango cha fedha za FBME ambacho kinashikiliwa na Benki kuu ya Cyprus ni takribani EUR 160,000,000. Matatizo ya Ukwasi? Tunadhani sio kweli. Je, bado anaendelea kudai kushikilia sehemu kubwa ya fedha hizi kama ulinzi wa Bima ya Amana wakati Benki ya FBME imekuwa ikilipa ushuru wake wa kila mwaka kwenye mpango wa bima nchini Cyprus tangu mwaka 2004? – Na pengine ni moja ya benki chache kisiwani kufanya hivyo.
Matumizi yake ya neno ‘zetu’ na wakati mwingine, ‘zangu’ kuhusiana na fedha za FBME ni ya kuogopesha na vinagongana na vitendo vinavyoashiria kuleta madhara kwa Benki ya FBME. Inaonekana kama kinyume cha ‘Stockholm Syndrome’ ambapo mateka anaishia kujihusisha na watekaji wake. Hapa ni mtekaji anayeonekana kujaribu kujionyesha kama mwathirika.
Kwa kawaida, kunatakiwa kuwe na mwongozo wa kuitaka Benki Kuu ya Cyprus kukabiliana na ukweli na kufanya kazi inazowajika nazo kama wasimamizi wengi wanavyotarajiwa kufanya kwa manufaa ya sekta ya benki, kwa maslahi ya wateja na pia – kwa manufaa ya Jamhuri ya Cyprus. Lakini tunahisi wanatingwa na mambo mengine tofauti kwa wakati huu.
Kujiuzulu kwa Msimamizi Maalum wa Benki ya Laiki iliyofungwa ikiwa ni matokeo ya kuingiliwa na Benki Kuu ya Cyprus ni kashfa inayokuja juu kwa sasa. Benki Kuu, inaonekana, ilisitisha uteuzi wake wa uwakilishi wa kisheria katika kesi ya kisheria dhidi ya mwenyekiti wa zamani wa Laiki. Uteuzi wao unaonekana kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa uhusiano wa nyuma na mwenyekiti wa Laiki – kiasi fulani kama mgongano wa maslahi uliokuwepo kwa Msimamizi wa kesi ya FBME. Barua ya kujiuzulu ya msimamizi Maalum wa Benki ya Laiki ya tarehe ya Jumatatu imesababisha dhoruba kwenye vyombo vya habari.
Je ni ajabu kwamba Benki Kuu ya Cyprus imepata tena alama ya pili kutoka chini ya heshima kwa umma katika utafiti uliofanywa kwa vyombo vya habari – Stockwatch, iliyochapishwa tarehe 31 Desemba 2014? Alama yake ni lazima itakuwa chini zaidi kwa sasa. Utafiti huu ulisababisha wasiwasi mkubwa hata Mjumbe wa Bodi ya Benki Kuu ya Cyprus, Stavros Zenios, aliwaonya kupitia blogu yake iliyochapishwa tarehe 1 Februari kwamba taasisi itaitumbukiza nchi katika majanga mpya kama itaendelea kuwa na tabia ya kizamani. Na wapinzani wakubwa ya mageuzi ndani ya Benki Kuu ya Cyprus – ni wasimamizi wandamizi wake yenyewe, aliandika.
Ni uharibifu wa kiasi gani zaidi kwa maslahi ya walipa kodi na sekta ya fedha Benki Kuu ya Cyprus itaruhusiwa kusababisha wakati inaendeleza uharibifu ka Ng’ombe Dume kwenye duka la China?