CBC Waruka Kadri Ukweli Unavyojiri

Machi 15, 2015

 Habari zilizofika FBME ni kwamba Jamhuri ya Cyprus katika Mahakama ya Usuluhishi ya ICC mjini Paris, inataka tawi la Benki ya FBME Cyprus lifungwe kwa misingi kwamba hakuna wanunuzi waliopatikana kununua tawi hilo. Kwa maneno mengine, kwa sababu azimio lililotolewa kwa kulazimisha na Benki Kuu ya Cyprus Julai mwaka jana halikufanikiwa kwa hiyo wanataka kunyang’anya leseni ya FBME. Wanaongeza ya kwamba wanataka kufanya hili sasa kwa sababu kufungwa kwake kutawezesha ulinzi wa bima ya amana kutumika na fedha za FBME zinazoshikiliwa na CBC (EUR 158,000,000) zitaweza kutumika kufanya malipo hayo.

Kinachoonekana hapa ni kwamba baada ya makosa yaliyofanywa Julai mwaka jana na Benki Kuu ya Cyprus yenyewe, sasa wanataka kuhalalisha makosa yao kwa kuleta maafa zaidi kwa FBME na wateja wake. Walitahadharishwa mara kadhaa mwaka jana kuwa Azimio la Amri halikuwa muafaka na pengine haramu kutumika kwa Benki ya FBME, ila sasa wanataka kumaliza sakata hili kwa kuliua kabisa tawi la Cyprus.

CBC pia wanadhani wanaweza kutumia fedha za amana za Benki ya FBME ‘kwa ajili ya ulinzi wa amana ya bima. Hawawezi. Mpango wa ulinzi wa amana nchini Cyprus unafanya kazi chini ya sehemu rasmi ya sheria, iitwayo Sheria ya Uanzishwaji na Uendeshwaji wa Ulinzi wa Mitaji na Utatuzi wa Mikopo na Mashirika Mengine ya 2013. Ni chombo kunachotumiwa na wote na kufadhiliwa na mabenki (pamoja FBME) na kimeundwa ili kuwalinda wateja. FBME imekuwa ikilipa michango yake kwa wakati na kwa ukamilifu kila mwaka kwa wakati wote iliposhiriki kwenye mpango huu, kama inavyopaswa kwa taasisi zote za ndani na nje ya Cyprus. Kwa ufafanuzi, Ulinzi wa Mpango wa Bima ya Amana unaanza kufanya kazi pale Benki inaposhindwa kujiendesha na pia kama haiendeshwi na mali za benki inayofilisika.

FBME haijashindwa kujiendesha, wala haipo kwenye hatari ya kufanya hivyo. FBME ina amana ya zaidi ya EUR bilioni 1.5, ambayo CBC anashikilia EUR 158,000,000. Tawi la Cyprus lina ukwasi usiopungua 103.5%, maana yake linaweza kuwalipa wateja wake wote bila, hivyo hakuna haja ya kuingia kwenye Mpango wa Ulinzi wa Amana.

Ni muhimu kukubali kwa CBC kuwa waliharibu sana wakati wa majira wa joto yaliyopita, lakini njia ya kurekebisha mambo haina maana kuleta madhara zaidi. Kuna njia nyingi mbadala kwa faida ya wateja, Benki na kwa heshima ya Cyprus kuliko hii inayopendekezwa na CBC kwa sasa. CBC anajua suala hili kwa ufasaha zaidi lakini kwa nini wanaleta madai haya? Kunaweza kuwa na sababu kuu kuliko hii.

Katika siku chache zilizopita, Bunge la Cyprus limekuwa likisikiliza shauri linalohusu vitendo na nia ya CBC kuhusiana na  utatuzi wa benki iliyofilisika ya Laiki na kesi yake kisheria dhidi ya Mwenyekiti wake wa zamani. Gavana wa CBC na Wakurugenzi wake wamekuwa wakihojiwa na kamati ya wabunge, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Cyprus ametangaza uzinduzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai katika suala hilo. Kumekuwa na wito kutoka kwa wabunge na vyombo vya habari Cyprus kutaka wajiuzulu katika nafasi za juu.

CBC inatapatapa. Siyo tu wanakabiliwa na madhara yanayoweza kusababisha upotevu wa mamia ya mamilioni ya Euro, lakini pia wanasumbuliwa na mgogoro tofauti kuhusu Laiki, ambao umemkumba Gavana na Bodi ya Wakurugenzi wa CBC, msimamizi na wanachama wa Mamlaka ya Azimio.

Mjumbe mmoja tayari ameshajiuzulu ambae ni Stelios Kiliaris, ambae ni mmoja wa Wakurugenzi wakuu wawili wa CBC na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi. Wakati akijiuzulu, alimshutumu sana Gavana wa CBC, wajumbe wengine wa Halmashauri na wasimamizi waandamizi, kwa madai ya uzembe.

Mapambano yataendelea.