Aprili 12, 2016
Mr Alekos Markides, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ambaye sasa ni mshauri wa sheria kwenye Benki ya FBME alifanya mazungumzo kwenye vyombo viwili tofauti vya habari; redio ya taifa CyBC (tar 12 Aprili) na MEGA Television (tar 9 Aprili) katika kukabiliana na uanzishwaji wa hivi karibuni wa Mfuko wa Ulinzi wa Amana. Alidai kuwa Benki Kuu imekosa mkakati na sasa inajaribu kukwepesha mustakabali mzima kutokana na jinsi walivyolishughulikia suala hili.
Hapa Chini ni baadhi ya mazungumzo hayo ambayo yamesambazwa kwenye vyombo vya habari vya Cyprus:
Kwenye Redio ya CYBC:
- Mr Markides aliishutumu Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kwa ukatili, uzembe na matumizi mabaya ya madaraka” akisema kuwa Benki Kuu ya Cyprus ameamua “kuiua” FBME badala ya kuomba ushahidi kutoka FinCEN baada ya kutoa ripoti yao Julai 2014 ambayo ilidai kuwa inatumika kusafishia fedha chafu.
- Mr Markides alishutumu kitendo cha CBC kufuatia uamuzi wake wa kufuta leseni ya FBME Desemba 2015, ambapo FBME ilikoma kuwa taasisi ya kibenki, na hivyo, CBC hawakuwa na mamlaka ya kuteua mfilisi. “Uteuzi wake ni kinyume cha sheria na kwa hiyo hatakiwi kuwepo,” alisema. “Ni kesi ya dhahiri kabisa ya matumizi mabaya ya madaraka”.
- Mr Markides alisema kuwa Benki Kuu ilijaribu kuifilisi Benki hii ya Tanzania kwa kuiomba mahakama ya Cyprus kutoa amri hiyo, ambayo wanasheria wa benki waliizuia. Alielezea kuwa hatua hiyo ni sawa na kuiomba mahakama ya Cyprus kuifilisi Benki ya Barclays PLC
- Akizungumzia kundi la watu ndani ya Benki Kuu “lenye nguvu kubwa,” aliendelea kusema: “Kwa kuangalia ya mfumo wa kibenki, wana nguvu zaidi kuliko bunge, wizara ya fedha na Rais wa Jamhuri kwa pamoja, watu wachache wasiowajibika kwa mtu yeyote, wanaofanya kazi pasipo uwazi …. Unaweza kuona matatizo yakijitokeza ambayo yanaweza kuiharibu Cyprus.. na kuongeza “Tunategemea uwezo wa watu ambao wameonyesha mapungufu katika miaka miwili au mitatu iliyopita”.
Kwenye MEGA TV:
- Mr Markides alisema kinachotokea sasa ni kupooza kutokana na amri na mtizamo mzima wa Benki Kuu kwa miaka miwili iliyopita kama Mamlaka ya Azimio. Aliwakumbusha kwamba Benki Kuu ilitoa amri ya kuliweka tawi chini ya azimio kwa lengo la kuuza shughuli zake: “Tangia siku ya kwanza tuliwaambia hawataweza kumpata mnunuzi, hakuna hata mmoja atakayekuwa tayari kufanya liwezekanalo ili anunue tawi wakati kuna vita vya kisheria na wamiliki wa benki wanapinga uhalali wa vitendo vyako. Hawakutaka kulielewa hili “.
- Mr Markides aliendelea, “Wamefeli vibaya. Hawa watu hawapo tayari kukubali kwamba wamefanya makosa. Kwao ‘nimefanya makosa’ haikubaliki. Hivyo, wameondoa azimio na kufuta leseni ya benki, kwa hiyo benki si benki tena. Kisha wakaenda mahakamani na kudai uteuzi wa mfilisi, si kwa tawi tu bali kwa Benki nzinma ambayo ipo katika nchi nyingine. “
- Kuhusiana na uanzishwaji wa Mfuko wa Ulinzi wa Amana Mr Markides alisema: “Wanawapa [wateja] Euro 100,000 wakati wao wenyewe walisema ilikuwa ni muhimu kutoa amri (decree) ili kulinda amana na wateja. Sasa hii ndiyo jinsi ya kuwalinda? Na kwa hatua inayofuata, wanakabiliwa [Benki Kuu] na kesi za kisheria ambapo itabidi wasubiri matokeo ya kesi hizo. Lakini kuja leo na kusema eti watatoa 100,000 sio ulinzi wa dhamana kama wanavyosema, bali ni dhamana halisi (wateja kujidhamini wenyewe), na kwa kweli ni chaguo la tatu, la kushindwa kabisa kwa mpango mzima wa Benki kuu tangu Julai 2014. “
Akijibu tuhuma za fedha chafu Mr Markides alisema: “Wenyewe [Benki Kuu] walifanya uchunguzi na kamwe hawakubainisha kwamba kulikuwa na utakatishaji wa fedha chafu. Hili hawalisemi, kwa sababu kuna ukosefu wa uwazi hapa, na kuna kesi dhahiri ya matumizi mabaya ya madaraka. Hili lilisemwa na Wamarekani na bado hatujui ni kwa ushahidi gani FinCEN walilizungumza. Linalofanana na hili, kuna taratibu nyingine za kisheria zinasubiriwa kwenye mahakama ya Marekani. “