Aprili 10, 2016
Kufuatia mfululizo wa vitendo viovu, vilivyo kinyume cha sheria, holela na kukosekana kwa uwajibikaji kwa Benki Kuu ya Cyprus ( “CBC”), na kutangazwa kulikocheleweshwa kwa kuanzishwa mfuko wa ulinzi wa amana Aprili 9, 2016 ni hoja ionayokaribishwa, lakini ni miezi 21 baada ya Mamlaka ya Azimio na CBC kuitekeleza dhidi ya Benki ya FBME ( “FBME”).
Hata hivyo, hii inatokea baada ya kipindi kirefu ambapo Msimamizi Maalum aliwanyima wateja fura ya kupata fedha kutoka kwenye akaunti zao kwa maelekezo ya CBC na kwa madhumuni yaliyotamkwa wazi ya kuweka fedha za kutosha katika Benki kulipia Mfuko wa Ulinzi wa Amana. Fedha ambazo CBC integemea zimekuwepo kwenye milki yao kwa zaidi ya mwaka mmoja na mazingira ambayo yangeruhusu ulipwaji wa fedha za mfuko wa amana yalikuwepo kwa muda mrefu sana. Ni makosa kusema kuwa hali ya kiuchumi ya FBME ndio sababu ya kuanzisha ulipwaji huo; ukweli ni kwamba fedha zinatosha lakini jinsi CBC ilivyolikabili vibaya suala lenyewe limewanyima wateja fursa ya kupata fedha zao, ingawa, wakati huohuo baadhi ya wateja wamekuwa na uwezo mkubwa wakupata fedha kuliko wengine. Wateja watakuwa na maswali matatu muhimu:
1 – Kwa nini sasa?
2 – Je wateja wamekuwa wakihudumiwa kwa usawa na usahihi na mamlaka ya udhibiti nchini Cyprus?
3 – Je, hali ya wateja ni bora kwa sasa kuliko pale ambapo hatua sahihi zingechukuliwa kuanzia Julai 21, 2014? (Tarehe ambayo Hatua za Azimio zilichukuliwa na taratibu walizozitumia CBC kwa mujibu wa sheria zilipoanza)
Mfuatiliaji yoyote wa vitendo vya CBC kwa kipindi cha mwaka mmoja atagundua mambo matatu yaliyo dhahiri: ukosefu wa uwazi, ukosefu wa uwajibikaji, na ukosefu wa uwezo wa kiutaalam.
Majibu ya maswali ya wateja ni kwamba hawakupewa huduma kwa usawa; Mpango wa Ulinzi wa Amana unaanzishwa ili CBC iweze kudai kuwa imetimiza majukumu yake kwa wateja na kukwepa kuanikwa zaidi kwa utovu wa nidhamu; na kuingilia kati kwa CBC na Mamlaka ya Azimio imekuwa na athari mbaya kwa wateja. Ukosefu thabiti wa umahiri wa CBC hauhitaji maoni zaidi.
Wateja watakuwa tayari wamekwishabaini kuwa CBC na Mamlaka ya Azimio wanawajibika kisheria hadi sasa. Kwa kuchukua hatua sasa, CBC inataka kujenga sababu dhaifu ili kukabili maamuzi yoyote yanayotegemewa kutolewa na mahakama kwenye kesi ijayo ya kufilisi ili kuficha na kukwepa makosa ya waliohusika kutokana na matendo yao ya takriban mwaka mmoja na nusu sasa. Ulinzi wa Amana za Wateja haijawahi kuwa ajenda muhimu kwa CBC kwa wakati wowote ule.