Agosti 22, 2014
Kuendelea kuzuia miamala kwenye tawi la Benki ya FBME Cyprus kumeleta malalamiko zaidi ya 1,000 yaliyoandikwa na ya maongezi kwa Msimamizi Maalum wa Benki Kuu ya Cyprus. Kilichoanza kama tone, kikageuka kuwa mafuriko na sasa kimekuwa tsunami. Mapendekezo yametolewa kwamba Msimamizi Maalum huenda alizidisha mamlaka yake chini ya Azimio Maalum tangu kuteuliwa kwake tarehe 21 Julai. Inasemekana pia kuwa amekuwa ni kiini cha kesi iliyoko mahakamani kama inavyosemwa na walalamikaji.
Wakati wa uteuzi wake Msimamizi Maalum alisema lengo lake lilikuwa ni kulinda wateja. Mwezi mmoja baadae, ni vigumu kuona jambo moja ambalo limefanywa kutimiza lengo hili!
Tatizo siyo hatua – au kutotenda katika suala la kutoa vibali – lakini pia kukataa kushiriki katika aina yoyote ya mawasiliano. Hii haimsaidii mtu – si wateja, si benki waambata, si wafanyakazi wa FBME na kwa hakika si heshima kwa Jamhuri ya Cyprus. Kwa muda gani mamlaka inaweza kuruhusu hali hii kuendelea? Aidha ni vigumu kuona kama hii inaisaidia Benki Kuu ya Cyprus.
Hakika Wakati umefika kwa wenye hekima kutafuta ufumbuzi ulio bora.