FBME yatoa wito ripoti ya upelelezi wa PWC itolewe

6 Agosti 2014

Benki Kuu ya Cyprus uliipa kazi kampuni ya kimataifa PWC kufanya uchunguzi katika sekta yote ya fedha katika mji wa Cyprus, ikiwa ni pamoja na FBME, uchunguzi ambao ulifanyika kutoka Juni 17 hadi Julai 4 2014.  Matokeo ya ripoti hii hayajatolewa kwa FBME, wala wanahisa wake, wala si kwa umma wa Cyprus, ambao inawezekana kuwa walililipia uchunguzi huo. Ripoti hii inapaswa itolewe.

Katika mikutano baina ya viongozi waandamizi wa FBME na Benki Kuu ya Cyprus walisema kwamba ripoti haikuwa na taarifa kubwa zinazohusu uzuiaji wa fedha chafu ulizotia wasiwasi wowote.