Akaunti zafunguliwa, Habari njema (mwishowe!)

Novemba 6, 2014

Leo, Novemba 6, 2014, akaunti zote zilizokuwa zimefungiwa kwenye tawi la Cyprus zimefunguliwa kwa amri ya Benki Kuu ya Cyprus.  Kwa niaba ya wote wanaohusiana na FBME Bank na FBME Limited – bila shaka na wenye akaunti pia – tungependa kutoa shukrani zetu kwa Benki Kuu na Msimamizi wake kwa kuchukua uamuzi huu.

Wamiliki wa akaunti zilizokuwa zimesimamishwa watatakiwa kupata tabu sawa na wateja wengine wa tawi la Cyprus – waje wenyewe kuchukua hundi itakayolipwa kwenye benki za Cyprus kwa kiwango cha EUR 10,000 kwa siku. Ila angalau wanaweza kupata fedha zao!

Kwa sasa inaonekana ni aibu kulalamikia kuhusu akaunti  zilizosimamishwa, ila itakuwa vizuri kujua kwa nini zilisimamishwa kwanza na kisha kufungiwa kwa miezi miwili. Hasa, wakati kitengo cha kuangalia fedha chafu cha Benki hakikuona sababu ya msingi ya kuzifungia na chunguzi nyingine tano zilizofanywa na Benki Kuu yenyewe hawakuona sababu ya kufanya hivyo.
Lakini, kama tunavyosema kwamba ni malalamiko tu. Ni vizuri sasa kuleta habari hizi njema kwa wateja wote wa tawi la Cyprus.