Juni 17, 2015
Ni wazi kuwa, pelelezi mbalimbali kuchunguza mwenendo wa Gavana wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na marafiki zake zimesababisha CBC kuonekana wabishi (kama tulivyobainisha awali) na sasa wanaporomoka, kukwama na kuhangaika huku na kule. Hii si hali nzuri kwa taasisi yenye ushawishi mkubwa katika nchi kuwa nayo.
Pia kuna uwezekano wa kutokea uasi unaosemekana kuwepo ndani ya taasisi, wakati watu mbalimbali ndani ya CBC wakisukumana kuwania nafasi endapo meli itapoteza nahodha wake na maafisa wengine waandamizi. wakurugenzi wasio watendaji waliopo CBC wako kwenye harakati mbalimbali, na mkurugenzi mtendaji aliyebaki, mchumi George Syrichas, anaeneza ushawishi wake kila kona.
Matatizo ya CBC ni makubwa: Gavana anachunguzwa na kamati ya Bunge juu ya mgongano wa maslahi unaohusishwa na madai dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Benki ya Laiki. Katika hatua nyingine, polisi walivamia CBC mwezi uliopita, na kuchukua kompyuta kwa ajili ya uchunguzi wa Gavana, Mkuu wake wa wafanyakazi na Afisa Uhusiano wa Umma anatafuta ni nani aliyevujisha taarifa ya akaunti za siri za benki kwa vyombo vya habari.
Mgawanyiko mkubwa kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Cyprus na Naibu wake umesababishwa na vitendo vilivyofanywa na Gavana wa Benki Kuu.
Kufuatia chunguzi kadhaa muhimu kuhusu matendo ya CBC wakati wa mgogoro wa sekta ya benki Cyprus mwaka 2012-2013, wito umetolewa kuichunguza taasisi hiyo na uwezo wa wafanyakazi wake. Stavros Zenios, mkurugenzi asiye mtendaji wa CBC ambaye aliachia ngazi Machi 2015, alidai katika kujiuzulu kwake kuwa wasimamizi wakuu na wa ngazi ya kati walikubaliana na madai yote ya mageuzi.
Na sasa, Benki Kuu imechukua hatua ya kuiagiza kampuni ya ushauri ya Ujerumani Roland Berger kufanya uchunguzi. Maelezo ya madhumuni ya uchunguzi huu hayajawekwa wazi kwa umma – kama kawaida ya CBC kwenye suala la uwazi – lakini ukweli kwamba kinachotokea sasa lazima kiwe muziki ndani ya masikio ya watu katika kisiwa cha Cyprus. Wote wanapaswa kusubiri kwa hamu taarifa kwa umma ya matokeo na mependekezo yake.
Kwa wakati huu, huku kukiwa na watu wasio na uzoefu katika uongozi ambao mawazo yao yamegubikwa na utata, CBC haikupaswa kujiingiza katika matatizo ya kuliendesha tawi la Benki ya FBME la Cyprus. Labda kati ya matatizo yote waliyonayo, hili linaweza kuwa ghali zaidi, kama si kwa CBC yenyewe, basi kwa walipa kodi wa Jamhuri. Kilikuwa ni kitendo kisicho cha lazima na kilichokosa uwajibikaji kilichofanywa kwa Mdhibiti Mkuu wa FBME nchini Tanzania au kwa wamiliki wa FBME. Na imekithirisha matatizo kwa CBC, tasnia ya Benki na kwa Jamhuri, na kwa upande mwingine imeharibu maisha ya watu wengi na afya za makampuni pia.