FBME Kitengo cha Kadi Chatangaza Kupunguza Wafanyakazi

Agosti 12, 2014

Je hii ndio kulinda wateja waliliomaanisha Benki Kuu ya Cyprus walipotangaza kuichukua Tawi la Cyprus? Nini hatma juu ya wafanyakazi 72 wa Kitengo Cha Huduma za Kadi, ambao wamepunguzwa kutokana na kusimamishwa kwa biashara yake? Kwa upande mwingine, hii ni matokeo ya moja kwa moja ya Benki Kuu na mdhibiti Maalum kwa kutoruhusu Benki ya FBME Benki kufanya miamala.

Watatu zaidi wameshauriwa kuwa watapunguzwa katika kipindi kifupi kijacho endapo biashara haitoweza kuendelea. Hii inawaacha 30 tu ambao watabaki kwa sasa kwa sasa.

Tarehe 11 Agosti Kitengo cha Huduma za kadi cha FBME kiliachisha ajira za wafanyakazi wenye thamani na kuaminiwa, ambao baadhi yao walikuwa na uzoefu wa miaka 20 ‘na kampuni. Ilifanya hivyo ilipokabiliwa na hali ngumu kutokana na matendo ya Benki Kuu. Biashara ilisimamishwa tokea tarehe 7 Agosti.

Wafanyakazi wote waliopunguzwa kazini wameelezwa na Utawala na watapokea stahili zao kamili kutoka FBME katika mishahara wa Agosti pamoja na malipo fidia yao kutoka Serikalini.

FBME inasikitika kwa dhati kuwa hali hii imelazimika kwa sababu ya kukosa uwezo wa kufanya kazi. Inatoa pole kwa athari juu ya wafanyakazi, familia zao na washirika wao. Wafanyakazi waliobaki wataendesha kampuni katika kipindi hiki cha mpito, huenda kwa lengo la kujenga upya uendeshaji.
Kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2002 ili kushindana katika masoko ya Cyprus na Ulaya, kwa kuwapa wateja wa ndani uchaguzi wa kiushindani dhidi ya mtoa huduma pekee, JCC card Systems. Kabla ya kusimamishwa Kitengo cha Huduma za Kadi cha FBME  kilitoa huduma mbalimbali za kadi, kutoa huduma  kwa washirika, wafanyabiashara, mabenki na wamiliki kadi duniani kote.
Cyprus sasa imerudi kwenye ukiritimba, soko la mtoa huduma mmoja.