Taarifa kutoka FBME Limited juu ya Kesi iliyopo Mahakamani

Agosti 8, 2014

FBME Limited, kampuni tanzu ya benki ya FBME, inasikitika kwa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Nicosia kwa kutozuia katazo la Mpito kukataza uuzaji wa tawi la Benki la Cyprus. Kampuni itatafuta fursa nyingine kupinga uuzaji huu ambayo inaouita Uvamizi wa Kihasama.


FBME inapinga uuzaji wa tawi la Cyprus ambao inauona  ni wenye nia mbaya katika kukabiliana na tangazo Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN, ripoti iliyotolewa tarehe 17 Julai. Uuzaji wa namna hii haufanyi chochote kuwalinda wateja wa Benki au kuondoa athari za msambazo kama ilivyodaiwa.

FBME inafanya kazi na washauri wa kisheria na wahasibu wa uchunguzi huko Marekani kufanya tathmini ya kina ya taratibu zake za kupambana na fedha chafu. Jaribio lolote na mamlaka ya Cyprus kuuza tawi itaonekana kuwa njia ya kuzuia uchunguzi huu kukamilika.

Mapitio yanahitajika ili kushughulikia masuala yaliyojitokeza katika tangazo la FinCEN la Ilani ya Mapendekezo na Ilani ya Matokeo.

Hali ya kifedha ya Benki bado ni nzuri sana inafuata taratibu zote za utoshelevu wa mahitaji ya Benki Kuu ya Ulaya. Wakati wa kutangazwa na Idara ya Hazina ya Marekani uwiano wa kifedha wa muda mfupi ulikuwa asilimia 104% ambayo inatosha kufidia amana zote.

FBME Limited iliongeza kuwa imesikitishwa, kwamba, baada ya wiki tatu alizokuwepo, Msimamizi Maalum hakuchukuwa hatua kuondoa utata mbaya inayoikabili FBME kwamba inakosa kuwa na Benki mwambata. FBME inazo Benki mwambata.