FBME Ltd yakanusha habari bandia

7 Julai 2017

 Hivi karibuni kuna nyaraka zimechapishwa katika vyombo vya habari na mitandao zikieleza habari na madai bandia yasiyo na msingi na ya uongo inayotuhumu makosa mbalimbali ya FBME. Sisi, kama FBME Ltd, tunakataa kabisa taarifa hizo na makala hizi pamoja na tuhuma maalum.

Kati ya madai yanayohusishwa na ukaguzi huru uliofanywa na wakaguzi, FBME Ltd ingependa kuweka wazi, ili kuweka kumbukumbu sawa kuwa ukaguzi wote wa ulioagizwa kufanywa na Benki na/au Wasimamizi wa Sheria wote wamekiri  FBME haijawahi kuhusishwa makosa. Kwa hali hiyo madai yoyote yatakayo kinyume na hapo yanapotosha kwa makusudi na ni ya uongo, kwa lengo la wazi la kujenga hisia ya uwongo kwa umma na rasmi.

Tunahifadhi haki zetu zote za kisheria dhidi ya chapa zilizotoka na vilevile chombo kilichotoa taarifa na ripoti za siri ambayo ni mali ya Benki kinyume cha sheria. FBME Ltd itachukua hatua zote za kisheria dhidi ya makala haya ambao wamechapisha habari bandia. Habari hizi za  bandia zina madhara mabaya kwa sifa ya Jamhuri ya Cyprus, Benki pamoja na wateja wake.