Kamusi ya maneno

Novemba 7, 2014

Kamusi ya maneno yanayotumika katika tovuti hii imeandaliwa ili kuwasaidia wasomaji kufuatilia maendeleo katika suala la Benki ya FBME:

Azimio la Amri: Sheria ya Mikopo na Mashirika Menine ya Cyprus ya 2013. Madhumuni ya Amri hii ni kuboresha mtaji wa benki zisizo na mtaji.

Matumizi Mabaya ya Amri: Wakati unabadili matumizi ya Amri iliyopo na kuamrisha tawi la Benki nyingine na kulifanya kama vile ni lako

Uvamizi: Wakati unajaribu kuuza biashara ya mtu mwingine, kwa mfano tawi la Benki, bila ridhaa ya wamiliki.

 Kuwalinda Wateja: Wakati unasababisha ugumu kwa wateja kutumia fedha zao, na kuwazuia kabisa maelfu wengine.

Kunyongwa: Kuzuia kampuni kutumia fedha zake yenyewe bila sababu inayoeleweka, na hivyo kuizuia kufanya malipo kwa washirika wake, mfano ‘Merchants’ na mwishowe kuilazimisha kusitisha shughuli zake.

Ukiritimba na bei zake: Wakati kuna kampuni moja pekee kwenye soko inayotoa huduma kwa sababu umelazimisha kusimamishwa kwa mshindani wake; kisha wewe, mimi, Serikali na watu wengine nchini Cyprus tunashuhudia bei za huduma zikipanda. 

Kupunguzwa Kazini: Kwa kampuni kusitisha shughuli zake, kutokana na matokeo ya Maamuzi uliyoyafanya, imelazimika watu kupunguzwa kazini na kuwagharimu wao, familia zao na nchi ya Cyprus.

Huduma ya kawaida ya Kibenki: Siyo kinachotokea kwenye tawi la FBME Cyprus

Mgongano wa Maslahi: Ni Kitu kisichojulikana nchini Cyprus

Stifado: Kitoweo cha Sungura wa Cyprus – au mkorogo sahihi ambao mdhibiti anaweza kujikuta yumo 

Kukwepa Wajibu: Kumlaumu mtu mwingine, mfano aliyepo Afrika, kwa matokeo ya matendo yako mwenyewe.

Usuluhishi: Hatua ya kupata ufumbuzi wenye busara kwa njia ya majadiliano na uchambuzi wa hoja za pande zote mbili.

Agizo: Ni kipi unachokisimamia wakati hufikirii kuwajibika kwa mtu mwingine yeyote,  au wakati Agizo lako linasimamiwa na wewe mwenyewe na marafiki zako wachache. Ni kinyume kabisa na maana haklisi ya usuluhishi. 

Kufungwa Kwa Tawi: Nini hutokea wakati unakwenda likizo bila kuacha mtu wa kuidhinisha malipo au kufanya maamuzi wakati haupo?

Kupokonywa: Wakati kampuni ya uma inapochukua mali binafsi kwa matumizi yake yenyewe. Itaendelea