Septemba 4, 2014
Wamiliki wa FBME Limited wameukaribisha kwa mtazamo chanya uamuzi wa kutohoa akaunti za wateja wa FBME tawi la Cyprus hatua aliyoitangaza Msimamizi Maalum tarehe 1 Septemba. Uamuzi wa kuruhusu baadhi wateja kupata fedha zao kiasi kisichozidi EUR 10,000 kwa siku ingawa kuna vikwazo katika utendaji wake.
Wanahisa wanaamini kwamba hii itasafisha njia ya kuelekea kwenye utaratibu wa kurudisha tawi kwenye udhibiti wa Benki ya FBME na Bodi yake ya Wakurugenzi, kwa faida ya wateja, wafanyakazi na Benki, na kwa heshima ya Jamhuri ya Cyprus kwa ujumla.
Pengine mwanzo umekwisha anza, lakini kuna maswali makubwa ambayo bado hayajajibiwa. FBME Limited, Kampuni tanzu ya Benki, inauliza kwanini mchakato huu umechukuwa muda mrefu, na kwamba azimio hili limekuwepo kwa muda wa wiki sita wakati ambao kumekuwa na fedha za kutosha kwa wateja wote. Aidha, kwa nini kiasi cha EUR 10,000 tu kwa siku ndio kiidhinishwe? FBME ina fedha taslimu kiasi cha dola billioni 1.7 zinazoweza kutosha kukidhi mahitaji yote ya wateja. Hatimaye, kwanini mipango hii imewekwa kwa utaratibu wa Benki moja tu – Benki ya Cyprus?
Kitu ambacho hakikuwekwa wazi katika tangazo la Mdhibiti Maalum wa Benki Kuu ya Cyprus ni kwamba kuna wateja wengi ambao hawakupewa nafasi ya kupata fedha hizi, ambapo wengi wao hawakutakiwa kuwa walengwa wa ubaguzi wa aina hii. Kwa hiyo suala lililojificha nyuma ya pazia la kuwapa fedha baadhi tu ya wateja ilhali wengine wananyimwa linahitaji kutafutiwa ufumbuzi. Je, tangazo la Msimamizi lilikuja kwa shinikizo la kuogopa kuharibu mahusiano kutokana na malalamiko ya watu badala ya mchango halisi kwa lengo la kuirudisha benki katika shughuli zake za kawaida? FBME Limited inamkaribisha Msimamizi Maalum kuuambia umma na kutengeneza utaratibu utakaowezesha kurudi katika hali ya kawaida, na ashiriki kikamilifu katika mchakato huo.
Hakuna shaka kwamba ucheleweshaji usiokwisha na mikataba ya hapa na pale inasababisha madhara yasioelezeka kwa wateja na kuharibu haiba ya FBME Benki na Benki Kuu ya Cyprus.
Zaidi ya hayo, mamlaka za Benki za Cyprus zimeanza kuilaumu Benki Kuu ya Tanzania kwa matatizo walioyasababisha wenyewe. Wenyewe wamekuwa wakimpuuza Mdhibiti mkuu wa Benki ya FBME aliopo makao makuu nchini Tanzania na Meneja Msimamizi wake, na kuendelea kuchukua hatua moja baada ya nyingine kinyume na kanuni zote zinazokubalika. Katika kesi za namna hii, lazima kuwe na uratibu kati ya Mdhibiti wa nyumbani na ugenini, lakini utaratibu uliochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus utaratibu huu haukufuatwa kabisa.
Hata hivyo, hatua ya kwanza imekwisha pigwa na Benki Kuu ya Cyprus kwa kulegeza masharti kwa fedha za baadhi ya wateja. Na hatua hii ni lazima ipongezwe – hata ikiwa kwa mkono mmoja – kwa kuonyesha kusonga mbele kutoka kwenye msuguano haribifu uliodumu kwa wiki sita. Labda hii inatuelekeza kwenye njia ya mabadiliko ya moyo – tunaishi katika matumaini! Ni muhimu kwamba ufumbuzi sahihi unapatikana. Katika suala hili, wakurugenzi wa FBME wapo tayari kufanya kazi kwa umakini ili kutafuta njia ya kuondokana na msuguano huu.
Ukweli wa Mambo
Tangazo na msimamizi Maalum ya Benki Kuu ya Cyprus tarehe 1 Septemba liliongezeka mjadala juu ya mbinu zilizotumika katika kutekeleza hatua za Azimio dhidi ya tawi la Benkii (katika kesi hii FBME tawi la Cyprus), na kutekeleza bila kupingwa, kumbukumbu au hata kuonyesha heshima kwa ofisi ya makao makuu, meneja wake wa kisheria au msimamizi mkuu wa Benki ya FBME, Benki Kuu ya Tanzania.
Hakuna wakati ambao mashauriano sahihi yalifanyika, licha ya majaribio ya mara kwa mara, kwa maneno na kwa maandishi, kutoka kwa Mdhibiti wa Makao Makuu. Benki Kuu ya Cyprus imekuwa ikitenda kama vile ina mamlaka kamili juu ya Benki nzima na hakuna wadau wengine wa kuzingatiwa. Vitendo vya hivi karibuni vilivyofanywa na Benki Kuu ya Cyprus na Msimamizi wake Maalum vimefanyika kinyume kabisa na matakwa ya Meneja Msimamizi kisheria wa makao makuu.
Ukweli mwingine usiopingika:
Ukweli: Tarehe 21 Julai Benki Kuu ya Cyprus ilitangaza uamuzi wake wa kuchukua tawi la Cyprus ili kuliuza. Msimamizi Maalum alichukua udhibiti tarehe 22 Julai. Hivyo kulikuwa na wiki nne kati ya mwanzo wa Azimio na kusitisha huduma SWIFT tarehe 18 Agosti. Kwa nini miamala haikuanza mapema katika kipindi hiki? Njia za SWIFT zilifungwa na Meneja Msimamizi wakati kupokuwa na jaribio na Msimamizi Maalum kuchukua fedha za FBME zilizoko kwenye mabenki waambata nje ya nchi na kutaka kuzihamishia Benki Kuu ya Cyprus. Hatua hii iliweza kuibua maswali.
Ukweli: Benki Kuu ya Cyprus tayari ina kiasi kikubwa cha fedha za wateja wa FBME, hivyo kwa nini wasitumie fedha hizo kuwezesha miamala kwa ajili ya wateja mapema? Hili ni swali Benki Kuu inaendelea kulikwepa.
Ukweli: Benki Kuu ya Cyprus inajificha nyuma ya tetesi kwamba hakuna benki mwambata kwa FBME, wakati tunajua kuna benki zipo tayari kutoa huduma hizo kitu ambacho tumekisisitiza mara kadhaa
Ukweli: Wakati Benki Kuu ya Cyprus inatetea matendo yake katika suala la kulinda amana na kutaka kuuza tawi kwa manufaa ya umma, matendo yake hayakuwa na mafanikio yoyote. Kinyume chake, yametumika tu kudhoofisha sifa ya Benki na ya Jamhuri ya Cyprus kama mahali ambapo hapafai kufanya biashara na, hasa, biashara ya kimataifa benki ya kibenki
Ukweli: Hakuna mtu anataka kuona upunguzaji wa wafanyakazi kwenye shirika lenye afya kwa kuwa ni uharibifu. Lakini tendo la kufungia Benki ya FBME shughuli zake lilileta athari ya janga la kukiua Kitengo Cha Kadi cha FBME. Uendeshaji ilibidi kusimamishwa na wafanyakazi 72 ilibidi kuachishwa – matokeo ya kusikitisha kwa Benki Kuu ya Cyprus kwa uamuzi wa kulazimisha Azimio juu ya tawi la Benki ilipoamua kutangaza kuwa inataka kuuza tawi la Cyprus la Benki ya FBME.
Labda ni vema Benki Kuu ingetoa maoni juu ya hili
Ili kuona tangazo la Msimamizi Maalum lililochapishwa Jumatatu, Septemba 1, 2014,
bonyeza hapa