Mahakama yaahirisha Kusikiliza Kesi ya Uuzaji

Septemba 16 2014

 Mahakama ya Wilayaya Nicosia jana iliahirisha kesi ambayo iliwasilishwa na wamiliki wa FBME ya kusimamisha uuzaji wa Benki kwa sababu faili la kesi hiyo liliwasilishwa mahakamani wakati huo. Ilifahamika pia kwamba serikali ya Cypus ambayo ni mshitakiwa kwenye kesi hii, walishindwa kuwasilisha utetezi wao kwenye muda ulipangwa. Masuala ya utaratibu yalizingatiwa na Mahakama imelipanga shauri hili kufanyika tarehe 29 Octoba, 2014. Benki kuu imerejea ahadi yake ya kutotekeleza Azimio lolote aukuingia mkataba wowote kuhusiana na uuzaji wa tawi la Benki hadi hapo hukumu ya shauri hili itakapotolewa.