Juni 11, 2015
(*Mabadiliko Yanapozidi, Mambo Hubakia Kama Yalivyo)
Barua kutoka kampuni ya sheria Limassol na kutumwa kwa wafanyakazi wa FBME kwa niaba ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na msimamizi wake kuwakumbusha wafanyakazi juu ya wajibu wao wasishiriki kwenye utoaji wa taarifa kwa vyombo vya habari na hasa kwa tovuti flani (inaweza kuwa tovuti yoyote). Kwa kweli inaeleza kuwa utoaji habari huo ni ‘uvujishaji’, taarifa ambao ni sawa na ‘Watergate’ au mapambano dhidi ya utawala wa kiimla.
Barua inatishia wafanyakazi na kwa maonyo, kufukuzwa kazi na hata hatua za kisheria. Mambo makubwa!
La kushangaza, wanasheria hao wamepeleka barua hiyo sio tu kwa wafanyakazi wa tawi la FBME Cyprus, ambao CBC ina uwezo flani wa kuwadhibiti, lakini pia kwa wafanyakazi wa Makao Makuu na ya wa ofisi ya uwakilishi ya Moscow ambao hawawezi kufukuzwa kazi ama na CBC au Msimamizi wake. Ukweli ni kwamba, msimamizi hawezi kumfukuza mtu yeyote. Hivyo ni nini hasa kinachoendelea huko?
Ni kweli kuwa wana wasiwasi flani kuhusu tovuti hii, www.fbmeltd.com. Ni vema kujikumbusha wenyewe kwa nini ilianzishwa. Kama mara nyingi tunavyo weka wazi, hii ilifanyika ili kuleta mwangaza kwa yale yanayofanywa na CBC wakato wao na mawakala wao wanpofanya mambo bila kutoa maelezo ya kwa nini walichukua hatua walizochukua na kuidhinisha hatua ya Azimio kwa FBME tawi la Cyprus, na kuhusu hatua za kulihujumu tawi, Benki na wateja wake tangu wakati huo. Walichokuwa wanasema ni kuhusu lengo lao la kuuza tawi na kwamba hatua yoyote waliyoichukua walikuwa wanawasaidia wateja.
Hawajawahi kutoa maelezo zaidi ya haya: hakuna mantiki kwa nini wateja walizuiwa kupata fedha zao; hakukuwa na mipango yoyote ya baadae; hakukuwa na uhakikisho wowote kwa wafanyakazi au wateja; hakukuwa na maelezo kwanini CBC walishikilia amana; hakukuwa na maelezo kwanini CBC waliamua kuzifungia na baadae kufungulia baadhi ya akaunti; hakukuwa na maelezo kwanini matendo yao yaliwafukuzisha watu kazi kwenye kampuni tanzu; hakukuwa na majibu yeyote kuhusiana na maombi ya FBME ya kufanya kazi kwa pamoja nk. Kwa kifupi, hakukuwa na uwazi na kwa hakika, hakukuwa na msaada wowote kwa uhuru wa kujieleza.