Taarifa ya Benki Kuu Yafafanuliwa

Agosti 29, 2014

Wakati wa jioni ya 28 Agosti, Benki Kuu ya Cyprus ilitoa taarifa kuhusu mgogoro juu ya tawi la Cyprus la FBME. Ilikaribishwa na wanahisa kama mchango wa mjadala – au angalau mwanzo wa mjadala.

Kwa mfano, ilikuwa ni vizuri kusikia kwamba Benki Kuu haina uadui na FBME. Hadi sasa, bado haijawa wazi na hisia iliyoanzishwa katika kipindi cha wiki tano tangu walipochukua tawi la Cyprus, na wakati ambao wao waliendelea kubaki kwa sehemu kubwa kimya kabisa kueleza malengo yao. Lakini kama hakuna uadui, ni kitu ambacho tunaweza kujenga na ni lazima kipongezwe.

Taarifa ya Benki ya Kuu ilisema: “Mara tu tatizo lilipogunduliwa, hatua ya Benki Kuu zilikuwa zimelengwa katika kurudisha shughuli za FBME tawi la Cyprus katika hali ‘shwari’ na kulinda maslahi ya wateja” Ni wazi kwamba ni wateja wachache sana kama hakuna kabisa watakaoona kama wamefaidika na ulinzi huu unaosemwa – Kutoweza kutumia fedha zao kwa wiki tano – ina madhara makubwa. Huku si ‘Kuweka mambo ‘shwari’kama wanavyodai.

Wanasema kwamba tatizo la miamala ni kutokana na malipo kukataliwa na benki mwambata za nje – sisi tunaendelea kujiuliza maswali kwa sababu yapo mabenki mwambata yanayotaka kutusaidia kufanya miamala. Pia wanasema kwamba matendo yao yanakwamishwa na wamiliki wa benki, nasi tunauliza kwa ‘jinsi gani?’ Tunahitaji kujua jinsi wamiliki wanavyozuia uwekwaji shwari wa tawi la Cyprus; tupatieni maelezo.

Benki Kuu ilitoa sababu tatu kwa nini miamala ya wateja wa FBME tawi la Cyprus inapata pingamizi.

Kwanza, walisema, tawi la Cyprus haliwezi kutumia mfumo wa malipo wa Ulaya (SEPA) kwa ajili ya uhaulishwaji wa fedha za Euro. Ni kweli kwamba awali taasisi za benki mwambata zilikataa kusaidia, lakini mwishoni mwa mwezi Julai taasisi nyingine kubwa ya Ulaya (benki ya CommerzBenki) ilikubali kufanya miamala ya euro. Tulipomshauri Msimamizi Maalum wa Benki Kuu, alikataa kabisa kuruhusu sisi kuanzisha mpango huu.

Pili, Benki Kuu iliandika kwamba njia ya mtandao wa SWIFT ilikuwa imesitishwa. Kwa mara nyingine hii ni kweli, lakini hii ilitokea tarehe 18 Agosti wakati Msimamizi Maalum wa Cyprus alipojaribu kuhamisha kiasi kikubwa cha amana za FBME kuzihamishia kwenye akaunti ya Benki Kuu ya Cyprus. Kutokana na kwamba Benki Kuu ya Cyprus tayari ina 114,000,000 Euro ya amana za FBME hivyo kwa nini wasizitumie hizo kufanyia malipo? Na kwa nini bado wanazishikilia? Na pia nini kilichotokea cha kutoruhusu miamala ya wateja katika kipindi cha wiki nne kabla ya Agosti 18?

Sababu ya tatu ya kutoruhusu malipo yaliyotolewa katika taarifa ni kwamba wamiliki wa FBME wamezuia matumizi ya amana katika benki nyingine. Kwa jibu sahihi tunawaomba wasomaji kurejea kwenye kifungu cha hapo juu.

Hatimaye, Benki Kuu ilisema wamiliki wa FBME walikataa kukutana, ingawa wanakiri kwamba wakati mkutano huo ukijadiliwa mbia mmoja alikuwa nje ya nchi na mwingine ilikuwa anaumwa. Wamiliki wote wawili wanahitajika kuwepo na hili iliwekwa wazi kwenye barua kutoka ofisi ya sheria ya Markide na Markide & Co LLC ambao Benki Kuu ilikuwa na mawasiliano nayo. Lakini wamiliki wapo tayari na daima wamekuwa na nia ya kufanya mkutano huo; ni kiasi tu cha kuupanga upya. Kila juhudi ni lazima ifanywe ili kutatua suala la tawi la Cyprus kwa manufaa wateja wa Benki, kwa manufaa ya Benki na kwa manufaa ya Jamhuri ya Cyprus.

Wanahisa wa FBME wanathibitisha nia yao ya dhati kufanya kazi kwa nguvu zote ili kupata ufumbuzi chanya si tu kwa jambo hili lakini pia kwa manufaa ya Cyprus nzima – sasa na katika siku zijazo.