Maswali yaumizayo yanayojirudia rudia

Oktoba 31, 2014

Vita ya kisheria katika medani ya kimataifa inaendelea baina ya wamiliki wa FBME Bank dhidi ya Benki kuu ya Cyprus kuhusiana na uamuzi wake batili wa uuzaji wa FBME- tawi la Cyprus. Yaliyojiri hivi karibuni ni kukamilika kwa ufunguaji wa kesi iliofanywa na wanahisa wa FBME, katika Mahakama ya Kimataifa ya Biashara, Paris. Benki Kuu sasa inatakiwa kutoa hoja za msingi juu ya vitendo vyake batili na vyenye uonevu kwenye Mahakama hiyo.

 

Ni muda muafaka kuyarejea tena maswali yale yasiojibika kuhusu Azimio lililochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus.

Swali la kwanza ni je azimio lililotolewa na Benki Kuu ya Cyprus lilikuwa na makusudio gani na je lilikuwa linafaa? Amri hiyo hasa inatakiwa itumike kwa benki ambayo haina fedha za kulipa amana zake, au kwa maneno mengine, benki ambayo inafilisika. Hali hiyo haijawahi wala bado haijaikumba benki ya FBME, benki ambayo inaweza kulipa amana za wateja wake na wadai wake pia; licha ya hayo benki bado inakidhi kwa hali ya juu viwango na taratibu za kimataifa za kifedha na wala si muflisi hata kidogo.i. Amri hii ilikuwa ni matumuzi mabaya ya sheria na yenye hila na ilitumika ili kupokonya benki ya FBME. Kwa nini walimchagua kuwa Msimamizi wa benki, mtu ambae alikuwa na uhusiano wa kibiashara na kampuni ambayo ilikuwa inafuatilia leseni ya kuanzisha benki nchini Cyprus ? Ni wazi waliona uwezekano wa mgogoro mkubwa wa maslahi – kama alivyofanya Mheshimiwa Christofides mwenyewe alipojiuzulu ghafla kutoka kampuni hiyo, muda wa wiki tangu kuwa Msimamizi FBME, barua yake ya kujiuzulu imejaa utata mwingi , kwani tarehe inaonyesha alijiuzulu kabla ya kuwa msimamizi, kitu amchacho si sahihi na kinaashiria udanganyifu. Bila shaka, anaendelea kumiliki kampuni ambayo inatoa huduma za ushauri wa kisimamizi kwa mabenki. Swali letu ni kwamba – je inakubalika kwake kutumikia mabwana wengi?

Swali jingine linalotia uchungu, ni je kuna sababu ipi iliomfanya Msimamzi achukue kipindi cha wiki tano kuanza kuwapatia baadhi ya wateja sehemu ndogo ya fedha zao ?
Na je ni sababu ipi iliomfanya, atoe kiwango cha EUR 10,000 kwa siku na kwa wale tu ambao waliopo hapa Cyprus? Je kwa nini akaunti nyingi bado zimefungiwa? Sababu iliyotolewa ni masuala ya sheria ambayo – wakati wahusika hasa hawajaona masuala hayo. Je inawezekana kuwa aliyatunga haya?

Je, kwa nini barua zilitumwa kwa mabenki yenye amana na fedha za FBME zikiwaelekeze wapeleke fedha hizo Benki Kuu ya Cyrus? Je Benki kuu nayo ilidhamiria kuendelea na hila zake za awali?

Kwa nini, kama mpango hasa ilikuwa ni kuwalinda wateja wenye amana benki, mbona hakuna mpango dhabiti wa kufuata na wenye muelekeo unaostahili kitaratibu za kibenki?

Je ni muda gani Msimamizi ataendelea kujilipa kutoka mfuko wa FBME Benki? Yeye anajilipa kazi ya siku nzima, wiki nzima, pamoja na kuwa na  mapumziko ! vilevile wakati huwa ameshatoka ofisini saa 9 bila maelezo yeyote.