Profesa wa Marekani: “Kujiamini kwa Kupitiliza” kwa FinCEN Kunahitaji Usimamizi”

Aprili 16, 2016

 

Akiandika kwenye tovuti ya Amerika Banker, Sharyn O’Halloran, Profesa wa George Blumenthal wa Uchumi Siasa na Profesa wa masuala ya kimataifa na ya umma katika Chuo Kikuu cha Columbia, aliandika kwamba katika vitendo vyake dhidi ya FBME ni wazi kwamba “… Kujiamini kupita kiasi kwa FinCEN kunahitaji uangalizi zaidi” kutoka mamlaka za Marekani. Aliyaelezea mapendekezo ya adhabu ya FinCEN kama ya “kibabe”, na kuonyesha “… mapengo ya dhahiri katika mchakato wake wa utawala na ukosefu wa vielelezo muhimu katika kutekeleza azma yake kwa FBME, (ambayo) inaonyesha kwamba FinCEN ‘walitembea wakiwa wamelala’ kuelekea kwenye maamuzi yaliyopangwa ya kutaka tu taasisi ifungwe “.

Aliongeza kuwa “… inaonyesha pia kwamba kwa FinCEN kuilenga mipaka ya benki ni kinyume cha katiba,” na anaamini kwamba kwa kupinga mashambulizi ya FinCEN, FBME “… ina kesi nzuri”. Makala kamili inapatikana hapa: http://www.americanbanker.com/bankthink/overzealous-fincen-needs-more-oversight-1080438-1.html