Mchawi – Bado anatafutwa

Oktoba 30, 2014

Kuna imani miongoni mwa baadhi ya watu kwamba iwapo utauliza swali mara kwa mara itafika hatua kuwa utapata jibu unalotaka. Ni jambo linaloeleweka kuwa mtoto akitaka kitu, mara kwa mara atauliza “Je naweza? Je naweza? Naweza? Yote hayo huyasema kwa  matumaini kwamba mzazi hatimaye ataridhia. Hili hatulitarajii kutoka kwa viongozi waandamizi wa serikali kufanya hivyo, eti?

Wasomaji wa tovuti hii wanaweza kuhisi ni nini tunakidokeza. Wakaguzi kutoka Benki Kuu ya Cyprus wamerejea Benki FBME tawi la Cyprus wiki hii, wataona nyaraka zilezile za awali na kuuliza maswali hayohayo kwa watu walewale. Hivi karibuni mwezi Juni na Julai ripoti ya PwC ilitoka ambayo ilikuwa imeagizwa na FBME. Kabla ya amri ya azimio la Marekani, wanahisa wa FBME waliambiwa kuwa benki haina tatizo ingawa ripoti haikuchapishwa.

Baada ya tangazo la FinCEN, baadhi ya viongozi wa Benki Kuu pamoja na PwC waliamua kuja tena na wakaanza kazi ya kupitia na kupekua mafaili. Tukio hili ni la pili. FBME haikuwahi kuambiwa chochote ama kizuri au kibaya, huenda ni kwa sababu wakaguzi walikuwa wakitafuta mabaya tu, hivyo kuona kimya pia ilikuwa ni habari njema. Ilipofika Septemba, wakaja kwa mara nyingine tena na walikuja kufanya utafiti mwingine ilipofika katikati ya mwezi Oktoba. Hakukuwa na matokeo, hakuna maoni, na kusema ukweli,wala hakukuwa na shukrani vilevile. Na sasa kwa mara ya tano katika miezi ya hivi karibuni, Benki Kuu na wataalamu wa wanaolipwa fedha za hali ya juu wametinga tena katika jengo la Kennedy Avenue na Askofu Mkuu Makarios III.

Haijulikana ni kiasi gani cha ushahidi – au kutokuwepo kwa ushahidi katika kesi hii – unatosha kwa ajili azimio maalum la Kamati ya Benki Kuu? Usemi wa ‘mchawi anawindwa’  inathbitisha na kuelezea mateso haya. Benki Kuu ni inataka kuhalalisha kuanzishwa kwa hatua yake ya uuzwaji wa tawi la FBME. Hatua hii imeondolea sifa ya Cyprus, imeharibu imani za wateja na pengine imesababisha ukimya mkali uliopo katika korido zenye madaraka huko Ulaya na Marekani. Uchunguzi wa siku 60 uliofanywa kwa ukamilifu na wataalam kutoka Ernst and Young kutoka Marekani, umekamilika na tayari taarifa ilishatumwa kwa FinCEN,  kutumia kampuniya sharia ya kimataifa, Hogan Lovells imeandikwa. Maoni ya umma yanapatikana kwenye tovuti hii, Benki Kuu ya Cyprus ilipaswa kutuuliza sisi na tungewapa nakala. Hii ingesaidia kuokoa kwao muda wote na matumizi ya fedha za walipa kodi.

 

Wangeweza pia kuchapisha ripoti ya wenyewe inayo jitegemea ambayo ilianzishwa mwezi Julai pamoja na PwC, au matokeo yeyote ya tafiti walizofanya baadaye. Tarehe 21 Julai Benki Kuu ya Cyprus ilichimba shimo lake mwenyewe kwa kutoa amri na azimio baada ya uteuzi wa msimamizi wake. Wameendelea kuchimba zaidi, na kujikuta wanaenda chini zaidi na zaidi. Inasemekana kuwa Viongozi waandamizi wanajutia azimio hili. Ni ukweli usiofichika kuwa iwapo imetokea kuwa umenasa kwenye shimo, wazo zuri ni kuacha kuchimba kama unataka kutoka!