Ufunguaji wa kesi wakamilika katika baraza la Usuluhishi ICC

Oktoba 29, 2014

Usuluhishi baina wanahisa wa FBME na Jamhuri ya Cyprus sasa unaweza kuendelea katika katika Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris baada ya FBME kukamilisja kuwasilisha kesi tarehe 28 Oktoba 2014.

Ombi la usuluhishi limekuja baada ya uamuzi wa uliochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus kutaka kuuza tawi la FBME Cyprus, kitu ambacho wamiliki wanadai ni uamuzi usio na huruma na batili.

Usuluhishi unahitaji makubaliano ya uwekezaji (sheria namba 399) yaliyo fikiwa Juni 5 2002 baina ya Jamhuri ya Lebanon na Cyprus yazingatiwe. Ibara ya 6 ya Mkataba huu inakataza utaifishwaji wowote wa mali ya wananchi wa nchi husika, na ibara ya 12 inatoa nafasi ya usuluhuishi  kwa ICC iwapo kutakuwa na mgongano.

Benki Kuu ya Cyprus ilipoanzisha hatua ya azimio la kuuza tawi la FBME Cyprus ilifungua njia hii kwenda ICC, moja ya mashirika yenye taaluma ya usulushishi inayo ongoza duniani.

Kinachotafutwa huko ni kuzuia kitendo cha  Benki Kuu na msimamizi wake walio msitari wa mbele katika uuzaji wa tawi la Cyprus ili mikataba ya uwekezaji ilindwe. Hatua hizi zimechukuliwa ili kuweka wazi ukiukwaji wa mkataba huu, hasa kutokana na kukosekana wala madai yoyote kuletwa dhidi ya Benki.

FBME Benk pamoja na wengi wasio na kosa lolote wameteseka kutokana na hatua hiyo iliochukuliwa na benki Kuu ya Cyprus. Mawasiliano tuliopokea kupitia tovuti hii yanaonyesha wazi. Maamuzi ya Benki Kuu hayajamnufaisha yeyote zaidi ya kuleta madhara kwa wateja na Jamhuri ya Cyrpus kama kituo cha biashara.