Februari 16, 2015
Miongozo ya Basel ni miongozo ya kina yenye mapendekezo yaliyotolewa kwa ajili ya mabenki makuu ili kuwasaidia katika kukabiliana na taasisi zilizo chini ya usimamizi wao ambazo zinakabiliwa na matatizo. Kamati ya Basel ilichapisha miongozo hiyo mwaka 2002 kwa ajili ya Usimamzii wa Mabenki na kurekebishwa mwaka 2014. Makala hii inaangalia thamani ya matumizi ya hiyo miongozo.
Lengo la Kamati katika kutoa mwongozo ni kuhamasisha viwango madhubuti kulinda sekta ya kimataifa kutokana na kufilisika. Miongozo mingi imepitishwa kuwa ni sheria ya Ulaya na inafuatiiwa na mabenki kuu duniani kote.
Karibia mabenki kuu yote yanasema yanafuata miongozo hii, kama ilivyokuwa kwa Benki Kuu ya Cyprus (CBC) hapo awali. Kwa bahati mbaya,imeonekana kutoitumia kwa miaka ya hivi karibuni. Habari zaidi kuhusu Miongozo na kazi ya Kamati ya Basel inapatikana kwenye tovuti ya www.bis.org.
Kurasa 65 za miongozo zinatoa mapendekezo mengi madhubuti ya nini kifanywe katika hali ambayo si tofauti na ile ambayo imeikumba FBME katika kesi yake. Ifuatayo ni mifano michache:
Hitimisho kuu ya muongozo inaweka wazi kwamba kitendo cha usimamizi kiundwe tu pale ambapo benki inaonekana kuwa ‘dhaifu’, na si kwa benki yenye nguvu kama vile FBME, ambayo ilikuwa na asilimia 104 liquid wakati Benki Kuu ya Cyprus ilipochukua usimamizi kwenye tawi la FBME Cyprus. Mwongozo 106 unasema kwamba ‘Katika hali ya kawaida ni wajibu wa bodi ya wakurugenzi na mameneja waandamizi wa benki, si msimamizi, ndio watakao amua jinsi benki itakavyo tatua matatizo yake. Hii ni wazi kuwa lilipuuzwa na CBC wakati ilipotoa Azimio na Amri yake juu ya tawi la FBME Cyprus siku za mbili tu baada ya kupata taarifa ya mgogoro. Amri hii iliiwezesha CBC kupokonya na kuipa uwezo wa kuuza tawi FBME Bank Cyprus. Wamiliki na bodi ya wakurugenzi wa FBME Benki hawakushirikishwa kamwe na CBC katika maamuzi yake tokea wakati ulipochukua usimamizi hadi sasa. Mbaya zaidi, haikumshirikisha msimamizi wa ofisi ya makao makuu ya FBME wala mamlaka ya juu katika kesi hii, yaani Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Hitimisho kuu la muongozo linaendelea kuongeza kuwa kama ‘msimamizi atahitajika kutenda, msimamizi ana njia mbalimbali za kuanza kuchukua hatua, lakini matumizi hayo lazima yawe kwa awamu’. Ni wazi kuwa, uamuzi wa haraka uliochukuliwa wa upokonyaji na kuuza tawi la Cyprus haukufuata utaratibu na ufafanuzi huu.
Mwongozo namba 110 inahusu uwezekano wa kutofautiana baina ya msimamizi kwa upande mmoja na wakurugenzi wa benki hiyo na mameneja kwa upande mwingine, kuwa na maoni tofauti kutokana na asili na uzito wa suala hilo. Mwongozo unapendekeza ‘kufanya tathmini kwenye kituo’ kama njia ya ufanisi zaidi ili kubaini kiasi kamili cha matatizo. Kutokana na hilo basi inafaa kuuliza kwa nini tathmini hii haikufanya kwa pamoja baina ya wawakilishi wa Benk, BoT na CBC? Tunafahamu kuwa hii imezuiliwa na CBC. Mwongozo 251 unaohusu masuala ya wafanayo biashara ya kuvuka nchi, inapendekezwa kwamba ‘wasimamizi wa nyumbani (katika kesi hii BoT) na msimamizi mwenyeji (CBC) ambao ni wasimamizi wa vikundi, washirikiane katika kupeana taarifa mbalimbali kwa ajili ya usimamizi wenye ufanisi wa makundi na vyombo vyake na pia kuratibu kwa ufanisi migogoro inapotokea ‘.
Mwongozo 252 unasisitiza juu ya hili na Mwongozo 254 unaelezea zaidi: “Msimamizi wa nchi mwenyeji lazima azingatie athari ya maamuzi yake juu ya mifumo ya benki katika nchi nyingine”. Mwongozo 255 unaweka wazi kuwa ni Msimamizi wa nyumbani (katika kesi hii BoT) ndio mwenye mamlaka ya kutangaza ufilisikaji, na si mamlaka za Cyprus.
Kuna mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Basel yanayohusiana na kukabiliana na hatua za azimio. Mwongozo 188 unasema ‘Azimio lazima lianzishwe wakati benki sio tena yenye kuleta faida au haina uwezekano wa kuwa na tena faida na haina matarajio ya kuridhisha ya kupona.’ Hii ni wazi, kwamba kesi ya FBME ilikuwa mbalina hali hiyo. Hiyo ndio Miongozo ya Basel inavyosema. Kwa taarifa: Sheria za Benki za Cyprus zilipitishwa mwaka 1997, ni moja ya sheria kongwe duniani zinazotumika. Ukilinganisha na Benki Kuu ya Tanzania, sheria yake ilifanyiwa marekebisho mwaka 2006.