Kitengo cha Huduma za Kadi Cha FBMEKufungua Malalamiko ya Ushindani

Februari 6, 2015

Usikilizwaji wa kesi ya malalamiko ulioanzishwa na Tume ya Ushindani ya Cyprus utaanza wiki ya mwanzo ya Februari 9 na inatarajiwa itafikia mwisho mwezi Machi. Hii inahusiana na matokeo ya uchunguzi ya Tume dhidi ya JCC Payment Systems Limited, wanahisa wake na benki nyingine zinazohusiana hasa na utoaji wa kadi za malipo na kuendesha huduma za malipo kwa kadi. Malalamiko yanahusiana na suala la kutumia hali ya msimamo wa kuzuia ushindani na kuvunja sheria ya Ushindani namba 3 na 6 ya Cyprus na Sheria namba 101 na 102 ya Mkataba wa Umoja wa Ulaya.

Itakumbukwa kwamba Kamati ya Ushindani ya Cyprus ilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari tarehe 30 Mei 2014 kwamba baada ya uchunguzi wa malalamiko walikuta kuna dalili za ukiukwaji wa sheria ya ushindani. Tume kwa sasa imewaita JCC na wadau wengine kuwasilisha utetezi wao dhidi ya matokeo yake.

Kesi hii imefunguliwa na Kitengo cha Huduma za Kadi cha FBME. Pamoja na ukweli kwamba Kampuni alilazimishwa kusitisha shughuli zake Agosti 2014 kutokana na hatua zilizochukuliwa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus, imeendelea kufuattilia malalamiko yake dhidi ya JCC, wanahisa wake na wengine.