Februari 9, 2016
Maoni ya Umma yamewasilishwa kwenye Idara ya Hazina ya Marekani FinCEN kufuatia Ilani yake ya Mapendekezo ya Hukumu dhidi ya Benki ya FBME. Haya yanafuatia ombi la FinCEN kutoka kwa jaji Cooper wa Mahakama ya Wilaya ya Columbia ya Marekani ili kuyapitia upya madai yake na mapendekezo ya hukumu.
Walipopewa ruhusa hii, FinCEN waliongeza kipindi kipya kwa ajili ya kuwasilisha maoni ambacho kilidumu hadi Januari 26 mwaka 2016. Wanasheria wa FBME wamewasilisha maoni yao ya Umma – yanayopatikana kwenye tovuti hii – na kumekuwa na idadi ya watu wengine ambao pia wametuma maoni yao, kama watu binafsi na kama wawakilishi wa makampuni/mashirika.
Upatikanaji wa maoni hayo ni kupitia tuvuti ya umma:http://www.regulations.gov/#!docketBrowser;rpp=25;po=0;dct=PS;D=FINCEN-2014-0007;refD=FINCEN-2014-0007-0057
Mmoja wa walioandika ni Profesa William H Byrnes, mtaalamu anayekubalika na anayeongoza katika somo la Kupambana na Fedha Chafu (AML). Katika uwasilishaji wake amesisitiza kuwa haya ni maoni yake mwenyewe na hayawakilishi shirika lolote ambalo yeye anahusiana nalo. Profesa Byrnes ni mhadhiri katika Chuo cha sheria cha Texas A & M, na mwandishi mahsusi wa mikataba mingi ya kisheria kuhusiana na kupambana na fedha chafu na ni mtu aliyetumia miaka 20 kutoa mihadhara juu ya somo hili.
Ameandika: “Kwa sababu ya uwezo wake chanya na wenye nguvu, nadhani ni muhimu kwa Kifungu cha Sheria No 311 kutumika sambamba na madhumuni yake maalum, ushahidi na masharti yake… Bila kuficha, mamlaka ya FinCEN chini ya Kifungu cha 311 hayapaswi kutumika vibaya au hovyohovyo.
“Kwa hiyo ninafadhaika kuona FinCEN inaonekana kukiuka Utaratibu wa Kisheria (APA), na pia utaratibu wa mchakato (Due Process), hasa katika mambo matatu: a) kwa kuzuia taarifa ambayo sio ya siri na wala sio ya binafsi, b) kwa kushindwa kufanya jitihada za ziada (ama kwa njia ya muhtasari, kutoa kibali kwa wakili mwenye mamlaka kupata taarifa hizo au kuwezesha maamuzi kufanyika kupitia mtu wa kati) ili kuondoa utata unaotokana na taarifa za siri ambazo zinaweza kuwa chimbuko la maamuzi ya FinCEN; na c) kwa kushindwa kutambua na kutathmini njia mbadala iliyo sahihi. Nategemea FinCEN watapata fursa kurekebisha makosa yake ya awali, na kuwataka kuchunguza ushahidi husika, mawasilisho, na sheria kwa macho safi na makini kabla ya kufikia hitimisho. ”
Profesa Byrnes anaendelea kusisitiza kuwa utekelezaji wa APA ni muhimu. Alizungumzia madai ya awali yaliyotolewa (Julai 2014) dhidi ya Benki ya FBME na FinCEN na kuandika: “Kwa uzito wa tuhuma zilizotolewa, vithibitisho vilivyotolewa na FinCEN vilikuwa vyepesi na vinavyokosa ukweli.”
Alitoa maoni kwamba wakati FinCEN imekubali kufichua mambo manne kama ushahidi, haikukubali kuweka wazi ushahidi mwingine, “… ambapo inaleta maswali zaidi kuhusiana na ushahidi wanaokataa kuutoa.
“Kujiamini kwa FinCEN kutotoa vielelezo vya ushahidi wanaoutegemea inaonyesha ukiukwaji wa sheria na ukandamizaji unaofanywa na Chombo cha Kisheria ambapo sheria za Marekani zimekuwa zikizikataa na kuzishutumu.”
Wakati hatua iliyopendekezwa na FinCEN ni ‘hukumu ya kifo’, Profesa Byrnes anaandika kwamba wathibiti wengine “… ni lazima watathmini ushiriki wao na FBME kutokana na uamuzi wa FinCEN, kama vile Benki Kuu ya Cyprus ilivyofanya kwa sababu zinazoonekana kuwa za uongo”.
Anaongeza: “ukali wa vikwazo vilivyopendekezwa kuwekwa na FinCEN, pamoja na kutopenda kwake kutoa taarifa zisizo za siri, inaonyesha tofauti kubwa kutokana na jinsi inavyoihukumu FBME dhidi ya benki nyingine kubwa ambazo zimefanya makosa mabaya zaidi.”
Kuandikwa kwa barua hii pamoja na watu wengine na fursa waliyopewa wanasheria wa FBME kuweka Maoni yao hadharani ni ushahidi wa harakati za Marekani kuweka haki na usawa mbele ya sheria, jambo ambalo mataifa yote yanatakiwa kuiga. Kipindi cha maoni kilimalizika tarehe 26 Januari, na ni wajibu wa FinCEN sasa kupitia upya maelezo yaliyotolewa, ushahidi ulio mbele yake, ikiwa ni pamoja na maoni yaliyotolewa na wahasibu waliochunguza taratibu za Kusafisha fedha (AML) za FBME, kwa lengo la kupitia upya maamuzi yake ndani ya siku 60 zijazo.
Fuatilia ukurasa huu! Tutawapa wasomaji taarifa ya maendeleo mapya.