Barua iliyotumwa kwa Benki Kuu ya Ulaya

Agosti 4, 2014

Wataalam wa uchunguzi kutoka marekani walianza uchunguzi wa ripoti ya iliotolewa na Idara ya Hazina FinCen.

Uchunguzi huo utakuwa wa uhakika na wenye ushirikiano. Kazi hiyo itakuwa maalum kuonyesha kuwa Benki inafuata misingi ya ukaguzi wa fedha chafu na Mtambue Mteja Wako.

Wanahisa wa FBME wamezuia zoezi la Benki Kuu ya Cyprus kuuza  tawi la FBME Cyprus wakati uchunguzi unaendelea.  Hii inaeleleweka na ndicho kinachohitaji na wote.

Hamna anae elewa kwa nini Benki Kuu ya cyprus iliingia kuongoza tawi la FBME Cyprus.  Wameleta madhara kwa kuzuia malipo kwa benki kama hii yenye afya. Msimamizi Maalum ya Benki Kuu ya Cyprus anadai  kwamba hii ni kutokana na kukosekana kwa mabenki mwambata, yaliyotolewa na Benki Kuu ya Cyprus, si kweli: kuna mabenki yapo.

Benki kuu ya Cyprus inadai inataka kuwalinda wateja lakini matendo yake yamekuwa kinyume.  Tanzania, mamlaka zimefika na kuruhusu shughuli ziendelee kote Makao Makuu na matawini.