BoT Yathibitisha haki Zake Kwenye Shauri la FBME

Agosti 23, 2014

Mdhibiti Mkuu wa Benki ya FBME, Benki Kuu ya Tanzania, inathibitisha haki zake katika usimamizi na udhibiti wa Benki ya FBME, miamala yote na matawi yake. Benki Kuu ya Tanzania imemteua Meneja Mwangalizi ambazo jukumu lake ni pamoja na kuruhusu miamala yote na shughuli zote zinazohusiana na Benki.

Meneja Mwangalizi pia alitoa maamuzi yake kuwa hakuna maelekezo yoyote yatakayofanyiwa kazi kuhusiana na Benki ya FBME bila ridhaa yake.