Mahakama Yaahirisha Uamuzi

Agosti 23, 2014

Usikilizaji wa shauri  juu ya Benki ya FBME kuhusu pingamizi la kuuza tawi la Cyprus , lililokuwa lifanyike Agosti 22, limeahirishwa na Mahakama Kuu ya Cyprus hadi 15 Septemba. Benki Kuu ya Cyprus imeahidi kutofanya chochote juu ya jambo hili kwa kipindi hiki.

Kiathari, ahirisho hili linatoa muda zaidi kwa uchunguzi kukamilika unaofanywa na wahasibu maalum.