Machi 20, 2015
Kuna ushahidi mkubwa wa matatizo yanayowakabili na watu wanaofanyia kazi makampuni yaliowekewa vikwazo ya utoaji wa EUR 200 kutoka akaunti zao FBME Cyprus. Kiwango hicho chenye ngazi ya EUR 200 kimekuwepo kwa ajili ya mashirika pamoja na watu binafsi tangu mwanzo wa mwezi Machi katika hatua ya kibabe iliyotungwa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus. Awali ilikuwa EUR 1,000 kwa siku.
Taarifa zinatufikia kwamba katika makampuni wanapata shida ila wanajitahidi kulipa wafanyakazi wao kwa wakati, hata kama kuna fedha za kutosha katika akaunti zao. Matokeo yake ni kwamba kuna madhara na ugumu kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao wenyewe. Ni wazi, hii ni kinyume na sheria ya mwaka 2007 ya masharti ya Ulinzi wa Mishahara.
Matatizo zaidi yanawakabili wateja wa makampuni katika malipo kwa ajili ya umeme, kodi, internet connection na huduma nyingine. Hii inaonyesha jinsi ‘sheria ya matokeo yasiyotarajiwa’ huathiri Jamhuri yenyewe, kuna athari nyingi sana yanayohusu malipo kwa kodi za mapato ya ndani, huduma za Jamii na Mfuko maalum michango kwa ajili ya waajiriwa wenye mishahara ya juu.
Malipo kwa siku kwa ngazi ya EUR 200 kutoka EUR 1,000 ilipunguzwa tarehe 3 Machi. Msimamizi wa benki aliweza kuweka punguzo katika kiasi, ngazi mbalimbali zilikuwemo na ngazi ya juu iliowahi kuwekwa ilikuwa EUR 10,000 kwa siku. Haikuwahi kamwe kuwekwa wazi mwanzoni kwa nini waliweka kikomo cha kila siku, wala sababu iliowalazimu wateja kuja Cyprus kupata umiliki wa hundi zao. Badala yake, Desemba mwaka 2014, msimamizi alitoa udhuru kuwa alikuwa akitafuta kushikilia kiasi kikubwa cha hifadhi kwa ajili ya bima ya ulinzi amana, ingawa sheria muhimu ya Cyprus inasema kwamba bima kama hio haiwezi kulipwa kutoka fedha za tawi lenyewe.
CBC kwa sasa inashikilia amana zenye thamani ya EUR 156 million- mali ya FBME. Tukiweka mahesabu, inastahili kukumbuka kwamba katika ngazi ya utoaji wa EUR 200 kwa siku kutakuwa na haja ya kuwa na jumla ya hundi 750,000 kwa ajili ya kuandikia malipo – hakika hakuna hundi za kutosha katika nchi yote ya Jamhuri! Tunaamini kwamba lengo la CBC haikuwa kamwe watu wa kawaida katika jamhuri na wateja wa FBME kupata taabu na tamko lake la azimio na Mamlaka yake.
Ni mtu mmoja tu, Msimamizi, ambaye haathiriki na zoezi la utoaji wa EUR 200 kwa siku, ambae hujilipa mwenyewe kutoka hazina ya FBME ya kiwango cha zaidi ya mara mbili ya kiasi cha kila siku ambacho yeye anaruhusu wateja wa Benki.