Tovuti Yaeneza Habari

Januari 30, 2015

Wakati wa mwisho wa miezi minne ya mwaka 2014, watu kutoka nchi 144 alitembelea tovuti hii, fbmeltd.com, karibia watumiaji maalum 58,000, huingia takriban mara 600,000. Hii inahusisha kipindi cha kuanzia Septemba 7, 2014 wakati tovuti ilipoanzishwa na baada ya kupatwa na mshtuko wa ‘kuingiliwa’, hadi mwisho wa mwaka. Kipindi cha awali kabla ya kushambuliwa, kutoka muda wa uzinduzi katikati ya Agosti hadi mwanzoni mwa Septemba, inaonekana kuwavutia wengi hadi kufikia watumiaji 100,000.

Ni wazi, tovuti imevutia wafuasi wengi wanaofuatilia. Ujumbe unaotutumwa kupitia ukurasa wa‘Wasiliana Nasi’ umeonyesha kuiunga mkono FBME, ingawa wengi wameonyesha ugumu na dhiki unaosababishwa na athari za Azimio la Amri na kukosa uwezo wa kupata taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vingine.

Shukrani zetu za dhati ziwaendee wote waliotuachia ujumbe na kutokubaliana na hali inayoonyesha kabisa kuwa ni  vitendo nya uvamizi

Kuenea kwa takwimu za upatikanaji wa tovuti ni jambo linalotia nuru. Ukiangalia uchambuzi wa anwani tofauti za IP, hakuna mshangao kuona kwamba idadi kubwa ya wanaoingia kwenye tovuti, 11414, wanatoka Cyprus. Uingereza ni ya pili ikiwa na 10,066, ikifuatiwa na idadi kubwa kutoka Russia, 6410, Amerika ya Kaskazini, 3062, Ufaransa 2157, Tanzania, 1695, Ukraine, 1576, Ujerumani 1066. Kwa ujumla, kompyuta 35937 tofauti ndani ya Ulaya( EU) zilitumika kutembelea tovuti katika sehemu ya mwisho ya 2014. Duniani kote, waliotembelea tovuti walitoka katika nchi 144, wanaowakilisha uwiano wa Umoja wa Mataifa na wa nchi zote kubwa.

Kama mameneja wa tovuti walivyotoa ripoti, idadi ya watembeleaji kutoka anwani tofauti za IP wanaweza jaza bwalo maalum la muziki la Sydney Opera House nchini Australia kwa ajili ya maonyesho ishirini na moja.