Uwakilishi wa Wanahisa wa FBME ‘ICC’

Desemba 3, 2014

Wanahisa wa FBME wamewateua washauri wa kisheria wenye uzoefu  mkubwa kwenye mahakama ya usuluhishi ya Kimataifa (ICC) mjini Paris, imetangazwa leo.

Ushauri wa kisheria utatolewa na Quinn Emanuel, akiongozwa na mshauri mwenza wa ofisi ya Paris, Philippe Pinsolle. Ameshawakilisha zaidi ya mashauri ya usuluhishi 200 ya kimataifa, akijikita zaidi katika mashauri ya Dola (Nchi) na wawekezaji pamoja na migogoro ya kibiashara. Amehusika kwenye usuluhishi chini ya mwamvuli wa karibu taasisi zote kubwa ikiwa ni pamoja ICC, LCIA, ICSID, SCC, AAA, ICDR, AFA, pia kwenye kesi za mara kwa mara chini ya sharia za UNCITRAL au vinginevyo. Philippe Pinsolle nae amewahi kuwa msuluhishi katika kesi zaidi ya 40, na vile vile kama shahidi-mtaalam juu ya usuluhishi na masuala mengine ya sheria nchini Ufaransa.

 Wanahisa wa FBME wamefungua kesi ya usuluhishi ICC dhidi ya Jamhuri ya Cyprus tarehe 28 Oktoba na kupitia usuluhishi inadai fidia kwa madhara yanayokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Milioni 500. Msuluhishi aliyeteuliwa na wanahisa ni Profesa Ibrahim Fadlallah, Profesa wa Sheria wa Emeritus katika Chuo Kikuu cha Paris. Profesa Fadlallah alishafanya kazi kama msuluhishi au mshauri katika usuluhishi wa kesi mbalimbali ndani ya ICC na vyombo vingine. Ni mwanachama wa zamani wa Mahakama ya Usuluhishi ya kimataifa ICC, mjumbe wa Baraza la Chuo cha Sheria ya Biashara cha ICC, mwanachama mwanzilishi baraza la usuluhishi la Ulaya na Arabuni (Euro-Kiarabu Forum on Arbitration) na mwanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya sharia.