Ripoti Ya Uchunguzi Yawasilishwa

Desemba 3, 2014

  Desemba 1, 2014 Benki ya FBME imewasilisha kwa FinCEN ripoti ya uchunguzi yenye maelezo ya kina iliyotayarishwa na wataalamu kutoka kampuni ya ushauri ya kimataifa E & Y (Ernst & Young). Aidha, Benki imewasilisha kwa FinCEN mamia ya kurasa za nyaraka kuhusu programu yake ya kupambana na fedha chafu na taratibu zake za ‘Jua Mteja Wako’ (KYC). Uwasilishaji huo kwa FinCEN ulifanywa na kampuni ya kimataifa ya sheria ya Hogan Lovells kwa niaba ya Benki ya FBME. 

Ijumaa ya tarehe 18 Julai 2014, ofisi ya FinCEN, Idara ya Hazina ya Marekani ilitoa Ilani na kuitaja Benki ya FBME kama ‘taasisi ya kigeni inayotakatisha fedha chafu’, na baadaye kutoa Taarifa ya Mapendekezo. Ilani ya Mapendekezo ya FinCEN haijakamilishwa na mamlaka za Marekani, na FBME inashirikiana na FinCEN kushughulikia masuala hayo ili Ilani hiyo iweze kuondolewa.