FBME Limited inakaribisha uamuzi kutoka ICC

Mei 25, 2015

Maamuzi ya hivi karibuni kwenye mchakato wa usuluhishi katika Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris yamekaribishwa na wamiliki wa FBME Limited. Wameeleza dhamira yao ya kutoa ushirikiano kamili kwa maamuzi ya mahakama hiyo na kufikia ufumbuzi wa mzozo kwa kushirikiana na washtakiwa.

 

Hasa hasa, wamiliki wa FBME wamekaribisha mwaliko wa pande zote zinazohusika katika mgogoro huu ili kuhakikisha kwamba tawi la Benki ya FBME la Cyprus halifilisiki au vinginevyo kuharibiwa, na kwamba hakuna hatua zaidi zitakazochukuliwa kudhoofisha maslahi ya wateja, wafanyakazi au wadau wengine.

 Wasuluhishi wameshauri pande zilizo kwenye mzozo kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta taratibu bora kwa ajili ya kuendesha tawi na kutatua matatizo kwa wateja, wafanyakazi, msimamizi wa mkuu na washirika wengine. FBME Limited imeanzisha juhudi za kuwafikia CBC sambamba na maamuzi yautaratibu wa Mahakama namba 3.