Matokeo Ya Hivi Karibuni Kutoka Mahakama Ya Usuluhishi ICC

Mei 21, 2015

Taarifa kwa vyombo vya habari imetolewa kuhusiana na hatua ya hivi karibuni ya Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris. Hii inahusiana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya hivi karibuni na inaweza kusomwa kwa kubonyeza hapa.

Usuluhishi katika Mahakama ya ICC unaendelea na maamuzi zaidi yanatarajiwa katika miezi ijayo. Tovuti hii itawapatia wasomaji – wafanyakazi, wateja, washirika na waathirika wengine – taarifa ya maendeleo.

Kesi ya usuluhishi ilifunguliwa na wamiliki wa FBME kwenye mahakama ya ICC tarehe 28 Oktoba 2014 kufuatia kuanzishwa kwa hatua ya Azimio na Benki Kuu ya Cyprus Julai 21, 2014 kwa kulipoka tawi la FBME la Cyprus, tawi lililokuwa na hali nzuri kifedha, na kujaribu kuliuza kinyume na matakwa ya wamiliki wake. Ombi la usuluhishi lilikuja baada ya kuona makubaliano ya kimataifa kati ya Cyprus na Lebanon yaliyoanza kutumika tarehe 19 Machi 2003 kukiukwa, ambayo yanalinda haki za mwekezaji katika kila nchi. Ibara ya 6 ya Mkataba huu inakataza kutaifisha au kupoka mali za raia wa nchi hizi, wakati ibara ya 12 inaruhusu usuluhishi, miongoni mwa njia nyingine za utatuzi.

Ikiwa ipo mjini Paris, ICC ni taasisi ya ulimwengu inayoongoza kwenye masuala ya utatuzi wa migogoro ya kimataifa na usuluhishi. ICC ina kazi kuu tatu: Kuweka misingi ya Utawala, Usuluhishi, na Uenezi wa Sera. Kwa sababu wanachama wake wenyewe ni taasisi zinazoshiriki kwenye biashara ya kimataifa, ICC ina mamlaka makubwa katika kuunda sheria zinazoongoza na kusimamia utekelezaji wa shughuli na mikataba kwenye nchi nyingi. Katika utangulizi wa kitabu chake juu ya Kanuni za Usuluhishi, ICC inaandika: ” Usuluhishi chini ya sheria ya ICC ni utaratibu rasmi unaopelekea maamuzi ya kisheria yasiyofungamana na upande wowote kimahakama, unaohusisha utekelezaji kwa mujibu wa sheria za ndani za usuluhishi na mikataba ya kimataifa kama vile Mkataba wa New York wa 1958 “.