FBME Yatoa Onyo la Hatua za Kisheria Hapo Baadae

Novemba 12, 2014

Wanahisa wa FBME Limited wameweka wazi kwamba wanaiwajibisha Benki Kuu ya Cyprus na watu kadhaa ndani ya Benki Kuu hiyo kwa uharibifu na hasara iliyoisababishia Benki ya FBME, wateja wake na wamiliki. Watu wanaodhaniwa kuwajibika ni pamoja na Msimamizi Maalum aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus kudhibiti uendeshaji wa tawi la FBME Cyprus.

Nia ya Benki Kuu ya Cyprus imekuwa kulipoka tawi la FBME Cyprus na kuliuza kwa wanunuzi wa nje kinyume na matakwa ya wamiliki wake. Nguvu ya azimio iliwekwa dhidi ya tawi la FBME Cyprus, hata hivyo nguvu za azimio hilo zilitakiwa kushughulikia taasisi zinazokabiliwa na matatizo ya ufilisikaji, na sio benki yenye fedha kama FBME.

Wanahisa wanatafuta ufumbuzi wa kisheria kwa matendo ya Benki Kuu ya Cyprus na msimamizi wake sambamba na mkataba wa ulinzi chini ya Cyprus,  Umoja wa Ulaya na sheria za kimataifa.

Tawi la Benki ya FBME la Cyprus limezuiliwa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus kuwasiliana na wateja wake, mabenki Mwambata na wengine kuhusu kinachoendelea., na ndio sababu ikaanzisha tovuti hii.

Mtu yeyote au kampuni inayotaka kununua tawi la FBME la Cyprus au mali anatangaziwa kwamba umiliki hauwezi kuhamishiwa kwao na mtu yeyote zaidi ya wanahisa waliopo. Uhamisho wowote kinyume na hapo utasababisha hatua za kisheria kuchukuliwa.