Afya ya Kifedha na Tunda la Tamu

Novemba 14, 2014

Ni takribani miezi mine sasa tangu Benki ya FBME tawi la Cyprus lilipopokwa chini ya Azimio na Benki Kuu ya Cyprus. Ni vyema kujikumbusha ya nini maana afya ya Benki na usimamizi wake wa fedha wa kihafidhina.

hapa Chini ni uwiano wa maeneo tofauti wa Benki ya FBME tawi la Cyprus kama tarehe 18 Julai 2014, kwenye ‘Urari mizania’ iliyotayarishwa na washauri wa ukaguzi K Treppides & Co Ltd:

Uwekezaji kwenye Mabenki Dhidi ya Amana = 84.15% Uwekezaji kwenye Mabenki na Hati za Dhamana Dhidi ya Amana = 104.44%

Jumla ya Mikopo Dhidi ya Amana = 15.95%

Mikopo Dhidi ya Amana 10.95%

Wakati hatua za Azimio zilipotangazwa, jumla ya amana zilikuwa USD 1.7 Bil. Ukwasi wa sasa wa tawi la FBME Cyprus na mabenk waambata  unafikia 96%.

Kinachoonekana hapa ni picha ya Benki bora, yenye ukwasi mzuri na inayopendeza kama tunda lililoiva mtini tayari kwa kuchumwa na mtu asiyeweza kuvumilia majaribu.

Kitendo cha Benki Kuu ya Cyprus kutaka kuchukua tawi la FBME Cyprus, kwa kutumia Sheria ya Jamhuri ya mwaka 2013 ya Azimio la Mikopo na Taasisi nyingine, na kisha kuliweka sokoni ilikuwa ni upokaji haramu na unyanyasaji ulio wazi wa sheria hii. Kama kisingizio, Benki Kuu alitoa ukosefu wa benki mwambata, ambayo ilikuwa si sababu ya kweli. Na pia ilitumia kigezo cha ripoti ya FinCEN ya Matokeo na mapendekezo ya matokeo, ambayo haikuwa sahihi. Na ilifanya hivyo baada tu ya siku mbili za kazi tangu kutolewa kwa ripoti ya  FinCEN. Ni wazi kabisa, ripoti ya FinCEN na suala la mabenki mwambata vilikuwa visingizio tu kwa Benki Kuu ya Cyprus kutafuta sababu ya kuuza tawi la benki yenye afya kifedha.

Baadhi ya takwimu zaidi zinaweza kuwa muhimu katika kuelewa matendo ya Benki Kuu na Msimamizi maalumu alieteuliwa nayo kuendesha tawi kwa amri. Chini ya mwezi mmoja baada ya uteuzi wake tarehe 22 Julai, Msimamizi alijaribu kuhamisha fedha zote za tawi la FBME na kuziweka chini ya udhibiti wa Benki Kuu ya Cyprus pekee. Alifanya hivyo kwa kuwaelekeza mabenki mwambata matatu  kuhamisha jumla ya amana za EUR 187,686,000 za FBME kwenda Benki Kuu, mchakato na kumpuuza mdhibiti mkuu wa FBME

Huu ni ukweli. Kulikuwa hakuna sababu kwa uhamisho huo, zaidi ya mchezo mchafu, ukizingatia kwamba Benki Kuu tayari inamiliki EUR milioni 100 za amana za FBME. Msimamizi pia alijua kwamba FBME itakuwa inachajiwa kiwango hasi cha riba au kuadhibiwa kwa kuweka fedha za ziada kwenye Benki Kuu ya Cyprus. Kwa bahati nzuri, hatua zilichukuliwa kuzuia maelekezo haya kufanyika.

Yote haya na matendo mengine ya mdhibiti yameendelea kuharibiwa thamani ya benki na kuwaathiri wateja wake.

Ukweli huu sasa unatazamwa kwenye mahakama ya usuluhishi wa kimataifa ICC mjini Paris.