fbmeltd.com Tovuti Yawafikia Wengi Duniani

Oktoba 10, 2014

Maelfu ya kompyuta duniani kote wanapata tovuti ya fbmeltd.com, kama inavyoonekana kwenye takwimu za hivi karibuni za matumizi. Idadi kubwa ya watu kutoka Amerika ya Kaskazini wanaipata tovuti hii na mara kwa mara huleta mrejesho. Wengine wengi katika EU na CIS pia ni wafuasi makini, pamoja na maelfu nchini Cyprus. Kwa ujumla, tangu tovuti ilipozinduliwa mapema Agosti kumekuwa na washiriki 425,000 binafsi kwenye tovuti kutoka nchi 79.

Tangu uzinduzi wa matoleo ya lugha mbalimbali  za Kigiriki, Kirusi na Kiswahili, ushiriki huu wa kimataifa unatarajiwa kupanuka mara dufu. Wasomaji wanaalikwa kutumia ukurasa wa ‘Wasiliana Nasi’ kutoa maoni yao juu ya nini kinaendelea, na mamia wamefanya hivyo, wengi wakitoa ujumbe wa nguvu wa kutuunga mkono..

Tovuti ya fbmeltd.com ilizinduliwa na wamiliki wa FBME Limited, ambayo ni kampuni tanzu ya Benki ya FBME. Madhumuni ya kuanzisha tovuti yakiwa  ni kutoa habari kwa umma kuhusu matukio nchini Cyprus na tuhuma juu ya nia ya Benki Kuu ya Cyprus kuhusu uamuzi wa kutoa Azimio dhidi ya Benki ya FBME tawi la Cyprus tarehe 21 Julai.

Nia iliyoelezwa na Benki Kuu, ikichukuliwa kutoka tovuti yake yenyewe, ilikuwa “kuuza shughuli za tawi kwa lengo la kulinda wateja wa FBME “. Tangu wakati huo imekuwa insha inayonyonga taratibu si Benki tu bali na wateja wake pia. Mwanzoni wafanyakazi wa FBME walidhani wangeweza kufanya kazi na Msimamizi aliyewekwa na Benki Kuu kuendesha tawi, wakagundua kwamba alifanya kazi kwa kiwango cha chini bila hata kusema. Kwa sababu yeye alizuia FBME Bank kuelezea wateja wake, waambata, wafanya biashara na waandishi wa habari nini kinachoendelea na wakati gani mambo yanaweza kubadilika, Kampuni tanzu ya Benki ilizindua tovuti hii ili taarifa iwafikie kupitia chombo cha umma

Msimamizi anaamini katika taarifa huru. Tunajua hilo kwa sababu alituambia hivyo. hakupenda maoni hasi yaliyotolewa kwenye tovuti ya fbmeltd.com yaliyotolewa kwake yeye na kwa Benki Kuu ya Cyprus, lakini daima anayo haki ya kujibu. Kauli alizozitoa tumekuwa na nia ya kuziweka kwenye tovuti hii na ni furaha yetu kufanya hivyo: kama anataka kuweka mtazamo wake au kama Benki Kuu ya Cyprus inataka kueleza kipengele chochote cha matendo yake, tutafurahi kuwapa bafasi kweny tovuti ya fbmeltd.com.