Arudia Tena!

Desemba 12, 2014

Je, hakuna mwisho wa kutowajibika na kiburi cha Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus? Amerudia kwa mara nyingine hila yake ya miezi michache iliyopita, na ametoweka bila kutarajiwa, kwenda kwenye mapumziko yasiyoidhinishwa. Kwa mara nyingine tena ameondoka bila kuacha mtu kwenye nafasi yake wa kuidhinisha malipo au mambo mengine yanayohusiana na tawi, na hakutoa tarehe ya kurudi. Hii imesababisha tawi kufunga shughuli zake na kuleta matatizo makubwa kwa wateja na wafanyakazi.

Siku ya Jumanne asubuhi, tarehe 9 Disemba, Msimamizi alisema alitaka kupitisha hundi na shughuli zote kufikia saa 7 mchana kwa sababu hangekuwapo siku inayofuata, yaani siku ya Jumatano tarehe 10. Jumatano ilifika na kuondoka, hata Alhamisi na Ijumaa Desemba 12 pia, bila Msimamizi kutokea au kujibu simu yake ya mkononi au hata simu nyingine zilizotoka kwa watu wengine ndani ya Benki.

Amekwenda wapi? Hakuna mtu ndani ya FBME aliyejua. Wala wale waliopo Benki Kuu ya Cyprus, angala kama hao wangeruhusu hali hii. Tunajiuliza, kwani amekwenda kufanya manunuzi ya Krismasi? Ni hakika kwamba ana fedha za kutosha baada ya kujilipa mshahara kwa kutumia fedha za tawi, shukrani kwa udikteta wa Benki Kuu ya Cyprus.

Jambo moja tungependa kuhakikishiwa ni kwamba hafanyi kazi kwenye biashara yake binafsi au kwa ajili ya taasisi yoyote nyingine. Mwongozo wa kazi yake unaeleza wazi kwamba haruhusiwi kufanya jambo kama hili akiwa Msimamizi wa tawi la Cyprus la Benki ya FBME na kama taratibu za siri za uendeshaji zinavyoelekeza.

Nikukumbushe tu kwamba, hajatoa kipaumbele kwenye swala la sheria na matakwa ya mamlaka yake hadi sasa!