Desemba 12, 2014
Kama ilivyvotajwa katika toleo la tarehe 20 Novemba kwenye tovuti hii, Ukwasi mpya, makosa yanazidi kujitokeza ambapo faini inatozwa kwa malipo ya amana za wateja wa FBME Bank kwa amana ambazo zinahitajika zilipwe na Benki Kuu ya Cyprus kwa sababu ya matendo ya Benki Kuu yenyewe . Kwa maneno mengine, Benki Kuu imeagiza FBME kufanya kitu, na baada ya hapo inaipa adhabu ya ushuru kwa kufuata agizo hilo!
Inastahili kujikumbusha kuna nini kilichotokea hapa.
Benki Kuu ya Cyprus imetayarisha toleo la kupikwa linalohusu Sheria ya Azimio, inayohusu mabenki ambayo yanakabiliwa na kufilisika, ambayo ingetumika dhidi ya tawi la FBME Cyprus – Benki moja ambayo, ilio na bado ina afya na inayojimudu sana. Ilivamia hilo tawi, akateuliwa Msimamizi ili adhibiti shughuli za tawi hilo na ilisema inaweza kuuza tawi na mali zake kama vile Benki Kuu ndio mmiliki wa FBME Benki. Hii ilikuwa tarehe 21 Julai 2014.
Septemba ilipofika, ilidhihirika wazi kuwa Benki Kuu haikuweza kuuza tawi wala kuwa na uwezo wa kuifunga tawi hilo tena. Hivyo, msimamizi wake aliruhusiwa kuja na moja ya mawazo ya kipuuzi: kuruhusu upatikanaji wa EUR 10,000 kwa siku, kulipwa tu kwa wale ambao ni wakazi au ambao wamekuja Cyprus. Ilipothibitika ngazi hiyo imara – hali hiyo ilijenga mazingira ya kusababisha benki kushindwa kujimudu – baadae wakabadilisha kiasi cha kuchukuliwa kila siku kote: kuwa EUR 5,000, na baadae kuwa EUR 2,000. Kiwango hichi cha mwisho kinaweza kulipwa kwa hundi kwenye benki moja tu mjini Cyprus. Kusudio la mpango huu ulifanyika ili ‘kulinda maslahi ya wawekezaji’ imeonekana!
Kutokana na mpango huo kiasi kikubwa cha amana za FBME inabidi kushikiliwa na Benki Kuu ya Cyprus ili kufanya malipo haya. Mbali na kiasi cha amana cha kisheria kinacho hitajika na mabenki yote na wasimamizi wao – asilimia moja ya jumla ya amana – EUR milioni 100 mali ya FBME zilipelekwa Benki Kuu. Mamilioni zaidi yaliongeza mwezi Novemba.
Hii ni wazi kuwa ni hali moja iliowekwa na Benki Kuu ya Cyprus kwa ‘maamuzi iliochagua wenyewe. FBME Bank isinge chagua kufanya hili, hata hivyo Bank isingeweza kujishirikisha kwa vyovyote kujiwekea vizuizi na kujiharibia njia ambazo zililazimishwa kwayo na msimamizi na wakuu zake katika Benki Kuu ya Cyprus. Hivyo haikutarajiwa kuwa kuna adhabu zaidi kwa FBME. Lakini hali hiyo ndio hasa kinachotokea.
Benki Kuu ya Ulaya ilitoa muongozo tarehe 5 Juni 2014 ukisema kwamba mabenki yanapaswa kuweka asilimia isiyozidi moja ya amana ya kisheria katika benki kuu. Lengo ilikuwa ni kuhakikisha kwamba wataweza kupata fedha zao na wataweza kujenga uchumi uliotikisika wa Ulaya. Kama kuna benki yoyote ilitaka kukimbiza fedha zake mbali na benki kuu ilistahili adhabu ya asilimia 0.2 itozwe kwa amana zote juu ya hiyo asilimia moja. Hili ni wazo zuri na moja ambalo lina faa kupongezwa.
Hakika hii haiwezi kufanyika kwa amana za FBME Bank katika Benki Kuu ya Cyprus? FBME haina cha kusema katika masuala ambayo mamlaka za Cyprus zimedhibiti katika Amri ya Azimio iliotunga binafsi. Hivyo, wao wanashtakiwa na kupewa adhabu.
Msimamizi wa Benki Kuu, Dinos Christofides, mtu anaehudumia mambo ya kawaida ya benki, anajua hili. Alisema kuwa ataenda kushawishi ili hii faini iachwe. Jambo ambalo bado halijatokea. Hata hivyo liko kwenye uchunguzi, hadi sasa tunaingia kwenye mwezi wa tano, hakika inaonekana kuna mtu ambaye si mkweli kuhusu tathmini hii. Ni wapi tulipowahi kusikia hili kabla?